The House of Favourite Newspapers

Hekari 807 Za Bangi Zateketezwa Mkoani Mara

0

 

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kushirikiana na vyombo
vingine vya dola, imefanya operesheni maalum mkoani Mara hususani katika kanda maalum ya
Tarime Rorya kwenye bonde la mto Mara. Operesheni hii, iliyofanyika kuanzia tarehe 02 hadi 08
Oktoba, 2023, imefanikisha uteketezaji wa jumla ya hekari 807 za mashamba ya bangi,
ukamataji wa gunia 507 za bangi kavu iliyo tayari kusafirishwa, gunia 50 za mbegu za bangi
pamoja na kuteketeza viwanda viwili vidogo vilivyokuwa vikitumika kuchakata na kufunga bangi
kabla ya kusafirishwa ambapo watuhumiwa 11 wanashikiliwa kuhusika na dawa hizo.
TUPATE TAARIFA ZAIDI
Akizungumzia wakati wa operesheni hiyo , Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na
Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo amesema, wakazi wa eneo hilo wamelifanya
bonde la mto Mara kama eneo maalum kwa ajili ya kilimo cha bangi na kujimilikisha kwa
kutoruhusu mtu yeyote asiye mkazi kuingia kwenye bonde kama sehemu ya kuficha uharifu
wao na wametishia kumdhuru yoyote atakayeingia ndani ya bonde hilo bila ridhaa yao. Pia,
wamediriki kufunga ofisi ya kijiji wakimtuhumu mtendaji wa kijiji cha Nkerege kutounga mkono
kilimo cha bangi.

Leave A Reply