Hemed Phd: Aliingia Kwenye Sanaa Kisa Kunyimwa Pesa na Mshua

Hemed Suleiman al maarufu kama Hemed Phd ni msanii wa muziki wa bongofleva na uigizaji wa filamu za bongo maarufu kama Bongo Movies.
Amezaliwa mwaka 1986 na kakulia jijini Dar es Salaam, alisoma Shule ya Msingi Oyesterbay na baadaye akahamia Shule ya Msingi Bunge kabla ya kujiunga na shule ya Sekondari Annuur Islamic baada ya kumaliza elimu ya kidato cha nne akajiunga na shule ya Eckeneford na baadae akahamia Coastal kwa ajili ya kumaliza kidato cha sita.
Ashiriki Tusker project fame
Baada ya kumaliza elimu ya kidato cha sita kipindi anasubiria matokeo akaamua kushiriki shindano la kusaka vipaji vya kuimba la Tusker Project Fame huko nchini Kenya. Shindano hilo lilimfungulia njia ya umaarufu Hemed kiasi kwamba akasahau masomo na kuacha kwenda chuo kikuu. Alishiriki shindano hilo na kushika nafasi ya kwanza.
Aanza kuigiza filamu
Baada ya kupata umaarufu aliamua kuingia kwenye sanaa ya uigizaji ambako aliamini kwamba angepata umaarufu zaidi. Aliigiza muvi nyingi zilizovuma kipindi hiko na kumpa umaarufu zaidi.
Akaigiza muvi nyingi akishirikiana na Jackline Wolper, Yusuf Mlela Jacob Steven au JB na mara kadhaa akaigiza na marehemu mzee Majuto. Kwa ushirikiano mkubwa wakafanikiwa kutengeneza filamu zilizoitambulisha vyema bongo muvi miongoni mwa wadau wa sanaa hiyo.
Pamoja na muvi pia akaingia kwenye uimbaji
Hemed licha ya kuonyesha kipaji chake kwenye uigizaji pia akaamua kuingia kwenye muziki na kuanza kuimba nyimbo za bongofleva.
Huku nako akajitahidi kwa kiasi kikubwa kuonyesha uwezo wake na waziwazi akalidhihirisha hilo kwa kutoa nyimbo kali kama vile ‘ Ninachotaka’ , imebaki stori, Carolina, Rest of my life. Nyimbo zote hizi zilifanya vyema kwenye soko la muziki ndani na mipaka ya nchi.
Anapenda sana wanawake
Mara kadhaa alipokuwa anahojiwa na vyombo mbalimbali vya habari Hemed hapepesi macho juu ya suala la kuwa yeye ni Mwendawazimu juu ya mapenzi na sio kwa msichana mmoja tu, yeye anadai anapenda sana wanawake na haipiti siku tatu bila ya kukutana na mwanamke.
Anasema kwenye maisha yake anapenda vitu viwili ambavyo ni kula sana na kwa siku anakula kuku wawili na nusu na kingine anachopenda ni wanawake.
Ana watoto sita, kila mtoto na mama yake
Hemed Suleiman ana watoto sita ambao kila mtoto ana mama yake, Hemed anasema mtoto wake wa kwanza ana miaka 3 na hao wamepisha kwa tofauti ya miezi miwili au mitatu. Anasema anawapenda watoto wake wote na muda sahihi utakapowadia atawaweka wazi kwa umma.
Anasema kuwa licha ya watoto hao mpaka sasa mchumba wake mmoja mimba ya mapacha iliharibika hivo basi angekuwa na watoto 8 katika umri wa miaka wa miaka 35.
Baba yake alikuwa mraibu wa madawa ya kulevya
Hemed anasema kuwa baba yake mzazi alikuwa ni mtu mwenye uwezo mkubwa wa kifedha lakini baadae akaja kuwa teja wa madawa ya kulevya na kuisahau familia yake kwa kiasi kikubwa na baada ya kuona hivyo ikabidi Hemed achangamke katika utafutaji na kuacha kutegemea mali za urithi wa baba yake.
Alikuwa na ndoto ya kuwa mtangazaji
Hemed Suleiman anasema kuwa katika maisha yake yote alikuwa na ndoto ya kuwa mtangazaji lakini ndoto zake zote zimekatika mara baada ya kuingia kwenye shindano la Tusker project Fame. Lakini hilo halijutii sana kwa kuwa sasa hivi mambo yake yanamwendea poa kwenye kazi yake ya uigizaji na uimbaji.

