The House of Favourite Newspapers

Hesabu Zaigomea Majimaji Ligi Kuu Bara

Kikosi cha timu ya Majimjai.

 

UONGOZI wa Klabu ya Majimaji, umesema hesabu zao za msimu huu za kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara zimegoma, hivyo hivi sasa wanapambana katika kuhakikisha hawashuki daraja.

 

Katika msimamo wa ligi hiyo, Majimaji inayodhaminiwa na Kampuni ya Sokabet ipo nafasi ya 15 katika ligi kuu ikiwa imecheza michezo 19 ikijikusanyia alama 15, ikiachwa alama 30 na vinara wa ligi hiyo, Simba wenye 45.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, meneja wa timu hiyo, Godfrey Mvula, alisema kuwa kwa sasa wamekwishakata tamaa ya kuweza kubeba ubigwa wa ligi kuu pamoja na kumaliza nafasi za juu, badala yake wanakazana kuhakikisha hawashuki daraja.

 

“Tumekata tamaa kwenye ubingwa, hii ni baada ya kupiga hesabu kwani tulikaa chini tukatathmini tukaona kwamba tutashindwa, hivyo nafasi yetu iliyobaki kwa sasa ni kuhakikisha hatushuki daraja kwa kuhakikisha kwamba tunashinda michezo iliyobaki,” alisema Mvula.

Comments are closed.