The House of Favourite Newspapers

HESLB Yaanza Kupokea Maombi ya Mikopo, Diploma Kunufaika – Video

BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imefungua dirisha la maombi ya mkopo kwa wanafunzi hao kwa mwaka wa masomo 2017/2018 huku ikiongeza idadi ya wanafunzi watakaonufaika na mikopo hiyo kutoka 33, 000 hadi 40,000 ikiwa ni ongezeko la wanafunzi 7,000.

 

Akizungumza na wanahabari, leo, Mei 10, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Abdurazaq Badru amesema maombi yataanza kupokelea leo hadi mwezi Julai wakati huohuo jumla ya Sh 437 bilioni zikiwa zimetengwa kwa ajili ya mikopo hiyo na mwaka huu pia bodi imeongeza wigo wa kutoa mikopo kwa wanafunzi wa stashahada ambapo hapo awali ngazi ya stashahada walikuwa wanapewa mikopo wale wa kozi za ualimu pekee ila sasa maeneo yenye uhitaji wa wataalam nayo yatapewa fursa hiyo.

 

“Mwaka huu kipaumbele kitawekwa kwenye kozi ambazo zina uhaba wa wataalam pamoja na zile zenye mchango katika viwanda. Katika kuhakikisha dhamira ya serikali ya kuwa Tanzania ya viwanda inatimia, tutaweka kipaumbele kwenye kozi ambazo zitazalisha wataalam, zikiwemo uhandisi wa gesi na mafuta, madini, Tehama, afya, kilimo na nyingine zenye uhitaji mkubwa,” amesem Badru.

HESLB Yaanza Kupokea Maombi ya Mikopo, Diploma Kunufaika – Video

Comments are closed.