The House of Favourite Newspapers

WEMA: Mobeto ni Mdogo Wangu, Lakini Mazoea Yamezidi – Video

Wema.

BAADHI ya wasanii wa Bongo Muvi walimuandalia hafla fupi msanii mwenzao, Wema Sepetu, wakimpongeza baada ya kushinda Tuzo za Sinema Zetu zilizoandaliwa na Azam TV mwezi uliopita ambapo usiku wa kuamkia leo ndipo shughuli nzima ilifanyika.

 

Wema aliwashukuru wasanii wenzake kwa hafla hiyo na kusema ameyasikia maneno ya baadhi ya wasnii walioponda baada ya yeye kupata tuzo hizo, lakini anazichukulia kama changamoto za kimaisha.

Mobeto.

Aidha, Wema amezungumzia uhusiano wake na Mwanamitindo, Hamisa Mobeto, ambaye awali alikuwa rafiki yake lakini baada ya kuzaa na X-wake Mbongo Fleva, Diamond Platnumz, urafiki umepungua kidogo.

 

“Hamisa ni kama Mdogo wangu, lakini kuna wakati sijui mazoea yakizidi sana kunaleta mushkeri kidogo, kwahiyo kila mtu anatakiwa kubaki kwenye mipaka yake,” amesema Wema.

MSIKIE WEMA AKIFUNGUKA HAPA

Comments are closed.