The House of Favourite Newspapers

Hii Ndiyo Hatari ya Diamond

0

Na Mwandishi Wetu, AMANI

Dar es Salaam: ‘Uswahilini’ kuna msemo kwamba, mwanaume au kijana rijali ni yule mwenye rekodi ya kutoka kimapenzi na wasichana wengi lakini mimi nakataa!

Kama ni kweli basi ilikuwa zama za kale lakini siyo zama hizi za vifo na  magonjwa. Hakuna mwanaume rijali wala kidume, bali staha ndiyo nguzo ya kila mmoja.

NAMUUNGANISHA DIAMOND

Makala yangu ya leo nimeguswa sana kumzungumzia Mbongo Fleva, Nasibu Abdul almaarufu Diamond.

Kumekuwa na habari kwenye vyombo mbalimbali vya habari, hususan magazeti kumhusu Diamond.

Licha ya uwezo wake mkubwa kwenye muziki wa kizazi kipya, dogo ni sukari ya warembo kwa maana ni  maarufu kwa kubadili wanawake.

HAPA NDIPO PENYE HATARI

Napenda kutumia makala haya kumwambia Diamond kuwa, umri wake ukilinganisha na idadi ya warembo aliotoka nao haviendani  kiasi kwamba, nikijaribu kumpigia mahesabu napata shida kuamini.

Diamond kwa sasa ana miaka 26. Ina maana kama uwezo wa kuanza kumudu kuwa na wanawake kama rijali, ni pale alipokuwa na miaka 18. Ukichukua 26 -18= 8.

Ina maana kwamba, Diamond kwa muda wa miaka 8 amekuwa na mzunguko mkubwa wa mademu. Mtungo wake unaonesha staa huyu ameshatoka na warembo 14!! Hapo achilia mbali wale ambao ilikuwa siri yake na hawakuwahi kuandikwa magazetini.

Kwa hiyo kwa hesabu za haraka, Diamond amekuwa na demu mmoja kila baada ya miezi kama kumi tu. Huo ni wastani wa jumla, hata kama kuna wengine alidumu nao kwa miaka miwili na wengine miezi mitatu.

KIAFYA IMEKAAJE?

Kila nikimfikiria Diamond, napata tabu kwani naamini umri wake (miaka 26) ni mdogo sana kwa kuwa na mzunguko mrefu kiasi hiki. Mbaya zaidi ni mzunguko wenye mizunguko ambayo nayo pia ina mizunguko. Sitaki kumchambua ila ukiangalia picha inajionesha kila kitu!

Niliwahi kuongea na mtaalam mmoja kuhusu afya ya mwanadamu, hasa katika umri mdogo na ngono! Mtaalam huyo aliniambia kwamba, uhusiano wa wapenzi wengi katika ujana unaweza kuwa na madhara mengine ya kivionjo yanayoweza kubadilisha mahusiano mazuri kuwa mabaya.

KINACHOONEKANA KWA DIAMOND

Mtaalam huyo alisema kijana anayependa kufanya tendo la ndoa mara kwa mara hujikuta akikosa msisimko haraka sana. Na hali hii humfanya asidumu katika uhusiano kwa muda mrefu na kuanzisha mpya kwa sababu ya kupoteza msisimko na yule wa awali.

MWILI KUTAWALIWA NA TAMAA

“Lakini pia tabia ya kufanya mapenzi mara kwa mara katika umri wa ujana huongeza uzalishaji wa homoni mwilini na kuufanya uwe na msukumo mkubwa wa kutaka kuridhishwa kwa tendo la ndoa bila kukosa na hivyo humfanya mhusika awe mtumwa wa ngono,” alisema mtaalam huyo.

HAPA KWENYE MAGONJWA SASA

Wanaofanya mapenzi holela mara kwa mara huwa katika hatari kubwa ya kuambukizwa magonjwa ya zinaa.

Kama Diamond hayupo makini (kwa kutotumia zana, lakini naamini ni makini) ina maana kwamba, anaweza yeye kuambukizwa au kuambukiza. Kama mrembo wake X alikuwa ana ugonjwa akampa yeye wakati huohuo akaachana naye, yeye akaanza uhusiano na mrembo Y, atampa ugonjwa ambao naye atausambaza tena na tena.

Hii ndiyo hatari ninayoiona kwa Diamond. Kwa hapa namsisitizia kuwa makini na kujichunga sana.

Leave A Reply