The House of Favourite Newspapers

Hii Ndiyo Simba, Mavugo Adai Hukumu Ya Yanga Imefika

SIMBA imejipanga kuhakikisha inaifunga Yanga leo na kuzidi kujikita kileleni ambapo kocha wake Joseph Omog amesisitiza kuwa, kikosi chake cha sasa ni cha ushindi na ndicho alichokuwa akikitafuta.
 
Kikosi hicho cha Omog raia wa Cameroon kipo kileleni mwa Ligi Kuu Bara kikiwa na pointi 16 katika mechi sita kikifuatiwa na Stand United yenye pointi 12 halafu Yanga inazo 10 tu katika mechi tano. Omog ambaye ameiongoza Simba katika mechi sita na kushinda tano akitoka sare moja, alisema: “Hii ndiyo Simba, tupo kamili kwa vita, Yanga naijua kuwa si timu ya kuidharau lakini sisi tupo vizuri zaidi yao. 
laudit-mavugo-simba-2016_112df1z9vgamx1p9udfi200uzd
Mshambuliaji wa Simba,  Mrundi, Laudit Mavugo.
 
“Wajiandae na kipigo kwani tumedhamiria msimu huu kuwa mabingwa na kurejesha heshima ya Simba iliyopotea kwa muda mrefu, nawaomba mashabiki waje uwanjani kwa wingi kutuunga mkono.”
 
Omog alisema ana imani kubwa na kikosi chake ambacho kiliweka kambi Morogoro kwa siku nne kujiandaa na mchezo huo kabla ya kurejea Dar es Salaam juzi wakati Yanga iliweka kambi Pemba hadi jana jioni. “Matokeo ya mechi zangu za nyuma yananipa nguvu ya kushinda mechi hii, naomba wachezaji wacheze katika viwango vyao tutafurahi,” alisema Omog. 
SIMBA DAY (2)  Kikosi cha timu ya Simba.
AKIWAKOSA MAVUGO, AJIBU ANAWEKA 
Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja, amesema safu yao ya ushambuliaji ipo vizuri na akishindwa kufunga Laudit Mavugo basi Ibrahim Ajibu atafunga leo.
SIMBA DAY (15)
Wakishangilia kwa pamoja.
 
“Takwimu zinaonyesha jinsi safu yetu ya ushambuliaji ilivyo imara kwa kufanikiwa kufunga mabao mengi, tumejiandaa vizuri kupata mabao kwa Yanga na wakijidanganya kumzuia Mavugo asifunge, Ajibu na wangine wapo na wanaiweza kazi hiyo,” alisema Mayanja, raia wa Uganda.
 
simba1
MAVUGO ADAI HUKUMU YA YANGA IMEFIKA
 Straika wa Simba, Mavugo akizungumzia mchezo wa leo, alisema: “Jumamosi (leo) ndiyo itakuwa hukumu ya Yanga kwa sababu nimejipanga kuwanyoosha na kuisaidia timu yangu kupata ushindi.”
 
1. Vincent Angban
2.Janvier Bukungu
3.Mohammed Hussein ‘Tshabalala’
4.Juuko Murshid
5.Method Mwanjale
6.Jonas Mkude
7.Shiza Kichuya
8.Muzamiru Yassin
9.Laudit Mavugo
10. Ibrahim Ajib
11. Jamal Mnyate
AKIBA: 1.Manyika Peter 2.Hamad Juma 3.Mohammed Ibrahim 4. Mwinyi Kazimoto 5.Novart Lufunga 6.Said Ndemla 7.Frederick Blagnon Imeandaliwa na Nicodemus Jonas, Sweetbert Lukonge, Said Ally na Omary Mdose.
 

Comments are closed.