The House of Favourite Newspapers

HOJA YA BABA NA DNA ZA WATOTO WAO YAIBUKA BUNGENI

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile amesema watu wanaoenda kupima vinasaba (DNA) kwa mkemia, wanakuwa tayari wana wasiwasi. Amedai kumekuwa na upotoshaji mkubwa katika jamii hasa katika suala la watoto ambao wengi wao huamini kuwa wanalea watoto ambao sio wa kwao.

 

“Si kweli kwamba watoto 6 kati ya wote tunaoishi nao majumbani kwetu siyo wa baba au wazazi husika. Takwimu hiyo ilikuwa inatokana na wale wazazi waliyokuwa wanaenda kupeleka vipimo vyao vya vinasaba ili kutambua uhalali wa mzazi, lakini haina maana kwa ujumla wetu Tanzania nzima watoto wengi hususani wakina baba kuwa sio wakwao hilo jambo sio la kweli”, amesema Dkt. Faustine.

 

Dkt. Ndugulile amesema lengo la kuweka sawa jambo hilo ni kutaka wabunge na wananchi wengine wanaume wasiweze kukimbia majukumu yao ya msingi katika malezi.

 

Naye, Naibu Spika, Tulia Ackson amefunguka na kuwakumbusha wanaume (kwa utani), kuwa hakuna umuhimu wowote kwa wao kufuatilia kipimo cha DNA ili kuweza kuthibitisha mtoto ambaye anamlea ni wake au laa, kwa madai kitanda hakiwezi kuzaa haramu.

 

“Nilidhani wanawake tunataka kuandamana humu ndani Bungeni, watu tuna watoto wengi humu lakini Kiswahili cha kawaida kabisa kinasema ‘kitanda hakizai haramu’ sasa unaenda kumpima wa nini?” amesema Tulia. 

 

KIPINDI CHA MASWALI NA MAJIBU BUNGENI

Comments are closed.