The House of Favourite Newspapers

Hostel Mpya za UDSM Kuanza Kutumika Wiki Ijayo

Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano chini ya Waziri Prof. Makame Mbarawa imesema kuwa mabweni ya wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) yaliyokuwa yakijengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) yapo katika hatua ya mwisho kabisa na kuwa yataanza kutumia wiki ijayo.

Wizara ya Ujenzi imetoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wao wa Twitter ambapo wameandika kuwa, “Mabweni yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 3,840 yaliyojengwa na TBA kuanza kutumika wiki ijayo.”

Mabweni hayo yalijengwa kufuati ombi lililotolewa na Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Rwekaza Mukandala kwa Rais Magufuli katika sherehe za uwekaji jiwe la msingi ujenzi wa maktaba ya kisasa chuoni hapo Juni 2 mwaka jana.

Akizungumzia changamoto za chuo, Prof. Rwekaza alisema kubwa ni makazi ya wanafunzi ambapo takribani wanafunzi 7000 wanaishi mitaani kwa sababu ya chuo kukosa mabweni ya kuwaweka wote.

Akijibu hoja hiyo, Rais Magufuli alisema tatoa bilioni 10 ambapo chuo kitenge eneo ambapo majengo hayo yatajengwa ili kupunguza idadi ya wanafunzi wanaoishi mitaaani.

Jumla ya majengo 20 yenye ghorofa nne kila moja yamejengwa katika eneo hilo la mashariki mwa chuo yatakuwa na uwezo wa kuchukua wanachuo zaidi ya 3,840 kati ya wanachuo 7,000 wanaolazimika kupanga vyumba vya kuishi mitaani kutokana na kukosa nafasi katika mabweni ya chuo yaliyopo.

TBA imetumia wataalamu na vijana wa kitanzania kwa gharama ya TZS bilioni 10 kukamilisha ujenzi huo ikilinganishwa na endapo ingetumia wakandarasi ambao walitaka kulipwa kati ya shilingi bilioni 50 na bilioni 100.

Comments are closed.