The House of Favourite Newspapers

HOTEL YA MAREHEMU ABDALLAH KIGODA YATEKETEA KWA MOTO

HOTELI ya aliyekua Mbunge wa Handeni mkoani Tanga marehemu Abdalah Kigoda inayoitwa Bwawani imeteketea kwa moto leo Ijumaa, Novemba 9, 2018, jioni, ambapo chanzo chake bado hakijafahamika.

 

Hoteli hiyo imeungua yote na hakuna kilichookolewa, ambapo baadhi ya mashuhuda walikuwepo hotelini hapo kwa ajili ya kuhudhuria mafunzo ya udereva wamelazimika kutoka nje kunusuru maisha yao walipoona moshi mkubwa ukitoka ndani ya hoteli hiyo.

 

Kwa mujibu wa Ofisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wilayani Handeni, Bi. Joani amedai kuwa mpaka sasa bado hawajajua chanzo cha tukio hilo na bado wanaendelea kuudhibiti moto huo usije leta madhala kwenye nyumba za majirani.

 

Kufuatia moto huo, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) wamezima umeme katika eneo hilo ili kudhibiti kusije kutokea athari katika maeneo ya jirani na makazi ya watu. Endelea kufuatilia taarifa zetu kufahamu zaidi.

RPC SHANNA Alivyokagua Ujenzi wa Kituo cha Polisi/ Atoa Kauli

Comments are closed.