The House of Favourite Newspapers

HOTELI BORA ZAIDI DUNIANI ZIKO CAMBODIA, ZANZIBAR

Viroth’s Hotel ya Cambodia inavyoonekana kwa mbele.
Taswira nyingine ya hoteli hiyo.
Mandhari ya nje ya hoteli ya Baraza Resort & Spa ya Zanzibar.
Bwawa la kuogelea la hoteli hiyo ya Baraza.
Moja vyumba vyake vyenye mvuto.

HOTELI bora zaidi duniani hivi sasa ni Viroth’s Hotel ambayo iko nchini Cambodia na gharama yake kwa usiku mmoja ni Sh. 250,000 (Paundi 78).

 

Hiyo ni moja ya hoteli 25 bora zaidi kwa mujibu wa tuzo za kila mwaka za taasisi ya TripAdvisor za Travellers’ Choice Awards kwa mwaka 2018 ambapo hoteli ya Bazara Resort & Spa, ya Zanzibar, ni miongoni mwake ikishika nafasi ya 25.

Viroth’s Hotel, iliyoko katikati mwa eneo la Siem Reap, katika kitongoji chenye shughuli nyingi cha Wat Bo, kina sanaa na madoido aina 50 ikiwa ni pamoja na bustani za chini na za juu ghorofani, vyumba 35 vyenye mvuto wa sanaa za hali ya juu, bwawa la kuogelea la mita 20, gym, kisima cha maji yenye kutia afya na mgahawa wa wazi ulio kando ya bwawa hilo.

 

Ushindi wa tuzo hiyo unatokana na mamilioni ya maoni na uhakiki uliokusanywa katika mwaka mmoja duniani kote kutokana na TripAdvisor.

Hoteli ya Baraza Resort & Spa iliyoko Zanzibar ni yenye huduma na hadhi ya nyota tano iliyo na malazi ya hali ya juu, uwanja wan je wa tenisi, chakula cha kila aina na bwawa la kuogelea na aina zote za mawasiliano ya kiteknolojia na habari.

 

Miongoni mwa vivutio vyake vikubwa ni vyumba maalum kwa ajili ya familia. Vilevile, hoteli hiyo iko mahali ambapo ni dakika 55 tu kuifikia kwa gari kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanziubar. Aina zote za michezo ya majini na kuogelea, inapatikana karibu na hoteli hiyo.

Orodha ya hoteli bora zaidi kwa kila kitu kwa 2018 duniani ni:

1. Viroth’s Hotel, Cambodia

2. Tulemar Bungalows & Villas, Costa Rica

3. Umaid Bhawan Palace Jodphur, India

4. Hanoi La Siesta Hotel & Spa, Vietnam

5. Gili Lankanfushi, Maldives

6. Hotel Belvedere, Italy

7. The Nantucket Hotel & Resort, USA

8. La Reserve Paris, France

9. Nayara Springs, Costa Rica

10. Hanoi La Siesta Hotel Trendy, Vietnam

11. Shinta Mani Shack, Camobodia

12. Kayakapi Premium Caves , Turkey

13. The Leela Palace Udaipur, India

14. Hotel 41, London

15. Baros Maldives, Maldives

16. Belmond Palacio Nazarenas, Peru

17. The Kilarney Park Hotel, Ireland

18. The Milestone Hotel and Residences, London

19. Hotel Estalagem St Hubertus, Brazil

20. The Oberoi, Mauritius

21. Aria Hotel Budapest, Hungary

22. Quinta Jardins do Lago, Portugal

23. The Tuscany, Turks and Caicos

24. Eden Rock, St Barths

25. Bazara Resort & Spa, Tanzania  

WALUSANGA NDAKI/MITANDAO/MASHIRIKA

Comments are closed.