The House of Favourite Newspapers

Museveni Amfagilia Rais Trump

RAIS wa Uganda, Yoweri Museveni amesema anampenda Rais wa Marekani, Donald Trump kwa sababu anasema ukweli mtupu kuhusu matatizo ya bara la Afrika na kwamba Waafrika wanatakiwa kuwa wamoja katika kutatua matatizo yao wenyewe.

Museveni amesema hayo katika hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Bunge la Afrika Mashariki jijini Kampala huku Balozi wa Uganda nchini Marekani, Deborah Malac akimkosoa Trump.

Maoni hayo ya Rais Museveni ni tofauti sana na viongozi wengi wanaochukizwa na kauli za Trump ambaye mapema mwezi huu alidaiwa kutoa kauli za kejeli kwa nchi za Afrika wakati wa mkutano wa kujadili masuala ya wahamiaji.

Trump alikanusha kutoa kauli hizo za kejeli lakini seneta mmoja aliyehudhuria mkutano huo alisema kuwa Trump alitamka maneno ya kejeli na matusi kwa nchi kama Haiti,Elsalvador na nchi za Afrika.

Kwa mujibu wa gazeti la New York times, mwaka jana Trump alisema kuwa watu wote wanaotoka Haiti wana UKIMWI, na wananigeria wakiruhusiwa kuingia marekani basi watakataa kurudi kwao ambapo Ikulu ya White House ilikanusha madai ya kauli hizo.

Comments are closed.