The House of Favourite Newspapers

Hoteli ya Mbowe Yadaiwa Kutumia Umeme wa Wizi

Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Mkoani Kilimanjaro limeikatia umeme hoteli  ya Aish hotel inayomilikiwa na Mbunge wa Hai (CHADEMA), Freeman Mbowe kwa madai kuwa wamebaini inatumia umeme wa wizi na kuisababishia Serikali hasara ya shilingi  milioni 10.8.

 

Akiungumza, Meneja wa Tanesco Mkoa wa Kilimanjaro, Mahawa Mkaka, Shirika hilo limebaini jana Septemba 14 kuwa wamejiunganishia umeme na kuharibu miundo mbinu yake.

 

“Baada ya kupata taarifa kutoka vyanzo vyetu tulienda kwenye hoteli hiyo kufanya ukaguzi,   tukabaini wameharibu mita na kujiunganishia umeme kinyemela. Hasara hiyo  ya milioni 10.8 ni kwa tathmini ya awali  na sasa hivi tunasubiri hesabu kutoka Tanesco makao makuu,” amesema Mkaka.

Comments are closed.