The House of Favourite Newspapers

Hotuba ya Waziri wa Fedha leo Bungeni

0

Mheshimiwa Spika, awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia uzima na afyanakuweza kukutana tena kwa ajili ya kupokea na kujadili kwa mara ya pilina kuidhinishaMapendekezo ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 2025/26kwa mujibu wa ibara ya 63(3)(c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniana kanuni ya 113 ya Kanuni za Kudumu za Bunge.

 

2.Mheshimiwa Spika, kwa namna ya kipekeena kwa masikito makubwa napenda kutumia fursa hii kutoapole kwa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Spika, Waheshimiwa Wabunge Wote, Chama cha Mapinduzi pamoja na Watanzania wote kwa kuondokewa na mpendwa wetu, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, aliyekuwaRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

 

Msiba huu umekuwa pigo na umeleta majonzikwa Taifa letu kutokana na uongozi wake mahiri, uchapakazi na uzalengo uliotukuka kwa Taifa. Mwenyezi Mungu ampumzishe mahali pema peponi,Amina.

 

Vile vile, napenda kutoa pole kwa Taifa kwa kuondokewa na Viongozi Wakuu, Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad, aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, na Balozi Mhandisi John Kijazi, aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi. Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema paponi.

KUSOMA HOTUBA YOTE FUNGUA HAPA => HOTUBAYA MHE. DKT. MWIGULU LAMECK NCHEMBA(MB.),WAZIRIWA FEDHA NA MIPANGO AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZOYA MPANGO WA TATU WA MAENDELEO WA TAIFA WA MIAKA MITANO 2021/22 2025/26

Leave A Reply