The House of Favourite Newspapers

Huddah: Kenyatta Halalisha Bangi

MSANII maarufu nchini Kenya, Huddah Monroe ‘amerusha kombora’ kwa Rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta,  akimtaka kuhalalisha matumizi ya madawa ya kulevya aina ya bangi kabla hata ya kura ya maoni kuandaliwa.

 

Huddah ambaye wengi wanafahamu kuwa anatumia mmea wa bangi kama kiburudisho chake, aliibuka na kauli hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram hivi karibuni na kuandika; “Kabla ya kura ya maoni, tunataka bangi ihalalishwe. Ni nani aliye karibu na rais kwa sasa? Mfikishieni ujumbe huu.”

 

Mwaka jana, zaidi ya Wakenya 1,400 waliunga mkono ombi la kutaka kuidhinishwa kwa matumizi ya mmea wa bangi baada ya mtafiti Gwada Ogot kuwasilisha hoja ya ombi lake mbele ya Bunge la Seneti na kubainisha kwamba matumizi ya kiafya  na utumiaji wa mmea huo viwandani unaojulikana kwa jina la sayansi kama Cannabis sativa,  una faida nyingi.

 

Alisema kuwa matumizi ya mmea huo yataimarisha hali ya uchumi,  lakini sheria nchini Kenya inapiga marufuku utumiaji wowote wa bangi na kwamba mtu yeyote atakayepatikana akitumia dawa hiyo atashtakiwa kwa uhalifu.

 

Mtafiti huyo ambaye amekiri kuvuta bangi wakati alipokuwa kijana,  amesema kuwa mataifa mengi katika bara Ulaya na Asia  na majimbo kadhaa nchini Marekani yamehalalisha utumiaji wa marijuana.

Ameorodhesha pia nchi za Colombia, Mexico, Jamhuri ya Czech, Costa Rica, Ireland, Australia, Jamaica na Ujerumani miongoni mwa nchi zilizohalalisha matumizi wa mmea huo.

Comments are closed.