The House of Favourite Newspapers

Huduma mpya ya usafiri Dar yazinduliwa

Meneja Mkuu wa Kampuni ya Usafirishaji ya LITTLE, Ashish Kukreti (katikati), Mjumbe wa Bodi, Abaas Mfundo (kushoto), na Meneja Uendeshaji wa kampuni hiyo, Jefferson Aluda, wakikata keki wakati wa uzinduzi wa huduma za kampuni  hiyo Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Usafirishaji ya LITTLE, Ashish Kukreti akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma za kampuni hiyo Tanzania katika hafla iliyofanyika JIjini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mkuu Mwendeshaji wa Kampuni ya Usafirishaji ya Little, Ashish Kukreti (kulia) akizungumza na baadhi ya wadau waliohudhuria uzinduzi wa huduma za kampuni ya usafirishaji  ya LITTLE jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau na wageni waalikwa wakifuatilia uzinduzi wa LITTLE Jijini Dar es Salaam.

 

Kampuni ya usafirishaji abiria kupitia mtandaoni ijulikanayo kama LITTLE imezindua huduma zake Tanzania zenye lengo la kuchangia katika kuleta suluhu katika adha ya usafiri.

 

Katika uzinduzi huo uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena iliyopo Posta jijini Dar es Salaam, ulihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo wadau wa usafiri na madereva.

 

 

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Little, Ashish Kruketi, alisema: “Kutokana na mahitaji ya huduma ya usafiri na kuongeza ajira kwa vijana katika Jiji la Dar es Salaam, tunayo furaha kubwa kuwatangazia kuwa tumezindua rasmi huduma hii jijini hapa.”

 

 

Naye Meneja Masoko wa Little, Katimpu Kisessa, alisema kampuni yao imeshasajili madereva 500 ambao wameshapata mafunzo ya huduma kwa wateja kutoka Little.

 

“Kampuni yetu imeanzishwa mwaka 2016 katika Jiji la Nairobi, kwa sasa ipo katika nchi nne ambazo ni Uganda, Kenya, Zambia na Tanzania.

 

“Sisi tumekuja kitofauti kabisa, siyo kama wengine, mteja anapoita usafiri wa gari, Bajaj au pikipiki, safari inapoanza basi ana uwezo wa kuangalia kiasi gani cha fedha anachotakiwa kulipa, lakini pia dereva na abiria wake tumewawekea ulinzi wa kutosha,” alisema Kisessa.

Comments are closed.