The House of Favourite Newspapers

Huduma Ya NBC Connect Yazinduliwa Mbeya, Kuboresha Huduma Za Kibenki

0
Mkurugenzi wa Kitengo cha wateja Wakubwa wa benki ya NBC Bw. James Meitaron (wa kwanza kulia ) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Benno Malisa ( wa Pili kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya NBC, Bw. Elvis Ndunguru (wa kwanza kushoto) na Mkurugenzi wa Bodi ya NBC, Dr.Kassim Hussein wakati wa uzinduzi wa NBC Connect , jukwaa la kidigitali la kisasa linalotoa huduma za benki kwa urahisi na salama, wkwa kutumia simu na vifaa vinavyotumia mtandao (Intaneti ).. Hafla hiyo ya uzinduzi ilifanyika jijini Mbeya.

MBEYA Mei 1, 2023: Benki ya Taifa ya Biashara ya (NBC) imezindua huduma ya NBC Connect, ikiwa ni ingizo jipya la huduma za kibunifu za kidijitali katika mkoa wa Mbeya.

Huduma hiyo ya kisasa ya kidigitali inalenga kuwezesha huduma mbalimbali salama za kibenki na ambazo huweza kufanyika sehemu yoyote, muda wowote kwa kutumia simu ya mkononi na vifaa vingine vinavyotumia Intaneti kwa mujibu wa Mkurugenzi wa wateja wakubwa wa benki hiyo, Bw. James Metairon.

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Benno Malisa akitoa hotuba kwa wageni waalikwa (hawapo pichani )wakati wa uzinduzi wa NBC Connect , jukwaa la kidigitali la kisasa linalotoa huduma za benki kwa urahisi na salama, wakati wowote na mahali popote kwa kutumia simu na vifaa vinavyotumia mtandao (Intaneti ). Hafla hiyo ya uzinduzi ilifanyika jijini Mbeya.

Akizungumza kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa huduma hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijiji Mbeya, Bw Metairon alibainisha kuwa kupitia NBC Connect, wateja wa mkoa huo na maeneo ya  jirani watapata fursa ya kuwa na uwezo wa kufanya miamala yao ya kifedha kwa urahisi zaidi na kupata uzoefu  mpya katika kupata huduma za kibenki.

“Huduma  hii itawapa wateja wetu uwezo wa kufanya aina zote za malipo ikiwa ni pamoja na malipo ya ndani na nje ya nchi, malipo ya Serikali pamoja na malipo kwa mitandao mbalimbali ya simu za mkononi kwa kutumia simu kompyuta au simu zao za mkononi.

Wateja pia wataweza kupata mwenendo wa miamala waliyofanya popote pale walipo pasipo kulazimika kwenda benki.’’ Alisema.

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Benno Malisa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa Benki ya NBC mara baada ya uzinduzi wa NBC Connect, jukwaa la kidigitali la kisasa linalotoa huduma za benki kwa urahisi na salama, wakati wowote na mahali popote kwa kutumia simu na vifaa vinavyotumia mtandao (Intaneti ).

Kwa mujibu wa Bw Metairon, NBC Connect imetengenezwa kwa teknolojia ya kisasa na yenye usalama wa hali ya juu ambayo imezibngatia na kutoa kipaumbele kwenye usiri wa taarifa za mteja. Ubunifu wa huduma hiyo kuhakikisha taarifa za kifedha za wateja zinalindwa wakati wote.

“Tunafuraha kutambulisha NBC Connect kwa wakazi wa Mbeya na maeneo ya jirani. Mfumo huu wa kibenki wa kidijitali ni uthibitisho wa dhamira ya kuwapatia wateja wetu huduma  bora za kibenki ambazo ni rahisi, salama, na zinazofaa na kukidhi mahitaji ya wateja. NBC Connect itawawezesha wateja wetu kufanya huduma zakibenki popote pale, wakati wowote, na kufurahia huduma hizo bila matatizo.” Aliongeza
“Pamoja na huduma rahisi na za kisasa, ujio wa huduma hiyo unatajwa kuwa utatoa usaidizi wa binafsi kwa wateja kupitia vituo vyao vya huduma kwa wateja ambapo kupitia mameneja katika vituo hivyo watawasaidia wateja kulingana na mahitaji yao na pia kutoa mwongozo wa jinsi ya kutumia jukwaa hilo kwa ufanisi.

Ili kusherehekea uzinduzi wa huduma hiyo jijini Mbeya, Benki hiyo ilitumia uzinduzi huo kutoa maelezo ya kina juu ya huduma hiyo kwa wateja waliokuwa tayari kujiunga na huduma hiyo ili kuwapa uelewa mpana wa namna ya kuitumia na kufurahia huduma hiyo.

“Tunawaalika wateja wetu wote wa Mbeya na maeneo ya jirani  wajionee urahisi na usalama wa NBC Connect. Ni huduma ambayo inaleta mapinduzi mapya katika namna ambavyo huduma za kibenki zinatolewa. Tuna uhakika  kuwa wateja wetu watufaika nayo kwa kiasi kikubwa , “aliongeza Bw Metairon.
Akiwa katika uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Bw  Benno Malisa aliishukuru Benki ya NBC kwa ubunifu wao mzuri na kuwahimiza wateja kutumia mfumo huo mpya wa kibenki ili kurahisisha shughuli zao za kila siku.

Zaidi, Bw Malisa aliushukuru uongozi wa benki hiyo kwa kuongeza tawi jingine katika mji wa Mbeya na kwa shughuli zake za uwajibikaji kwa jamii ambazo utoa mchango mkubwa kwa wananchi wengi nchini kote.

“Uzinduzi wa NBC Connect jijini Mbeya unawakilisha mpango mkakati wa upanuzi wa benki ya NBC ili kuwafikia wananchi wengi zaidi  na kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi.’’ Alisema.

Bw Malisa alionyesha kuguswa zaidi na dhamira kubwa ya benki hiyo katika kuwajibika kwa jamii kupitia mipango mbalimbali, kama vile Mbio za Kimataifa za NBC Dodoma zinazohamasisha na kutibu saratani ya shingo ya kizazi, msaada wa afya ya uzazi kupitia kliniki zinazotembea, programu za elimu ya kifedha, uwezeshaji wa vijana.

“Kupitia udhamini wa Ligi Kuu ya NBC mbali na kuongeza ubora wa ligi yetu na kuongeza burudani kwa watanzania udhamini huo umeongeza fursa za ajira kwa vijana na maofisa wengine wengi wa vilabu husika. Hakika napongeza juhudi hizi zinazofanywa na NBC” alisema Bw Malisa.

Uzinduzi wa NBC Connect jijini Mbeya unakwenda sambamba na uzinduzi wa tawi jipya lililofunguliwa katika soko la Mwanjelwa litakalotoa bidhaa na huduma mbalimbali za kibenki, zikiwemo akaunti binafsi na za biashara, mikopo, akiba na uwekezaji, huduma za fedha za kigeni na kidijitali.

Wateja pia watapata wataalam wenye uzoefu wa benki ambao wamejitolea kutoa huduma za kibenki za kibinafsi na zenye ufanisi ili kukidhi mahitaji ya kifedha ya jamii.

Leave A Reply