The House of Favourite Newspapers

Hukumu Kesi ya Morrison CAS Yasogezwa

0

MAHAKAMA ya usuluhisho masuala ya mpira kimataifa ‘CAS’ imesogeza mbele hukumu ya kesi kati ya klabu ya Yanga dhidi ya mchezaji Benard Morrison iliyokuwa isikilizwe Agosti 24,2021.

 

Kupitia taarifa rasmi iliyotolewa na CAS ikisainiwa na mshauri wao, Caroline Fischer imeomba radhi kwa pande zote mbili na kusogeza kesi hiyo mpaka Septemba 21,2021.

 

“Kwa niaba ya Rais wa mahakama ya usuluhisho (CAS) tunaomba pande zote mbili zipokee samahani ya kuchelewa kwa kutolewa rasmi maamuzi ya kesi, bado inafanyiwa kazi kwa kutoangalia upande wowote,”imesomeka taarifa hiyo iliyoandikwa na Fischer.

 

Leave A Reply