The House of Favourite Newspapers

Hulk Amtosa Mkewe, Aanzisha Mahaba na Ndugu Yake

0

STRAIKA wa Kibrazil, Hulk, ametoa kali ya kufungia mwaka, baada ya kuamua kuachana na mkewe wa ndoa iliyodumu kwa miaka 12, Iran Angelo de Souza na kuzama katika penzi la ndugu wa mkewe huyo.

 

Hulk na Iran waliachana rasmi Julai, mwaka jana na sasa straika huyo mwenye umri wa miaka 33 anayeichezea Shanghai SIPG ya China, kazama kimahaba na mpwa wa Iran, Camila.

 

Mwakilishi wa straika huyo wa zamani wa Brazil, amethibitisha uhusiano kati ya gwiji huyo na mrembo Camila, akieleza kuwa mahaba yao sasa hayajifichi.

 

Taarifa ilisema: “Hulk aliwaita wazazi na ndugu wa Camila na kuwaeleza ukweli. Walianza kutoka kimapenzi Oktoba. Ni Hulk mwenyewe aliyeitangaza ishu hiyo kwa sababu hakutaka kuficha kitu.”

 

Camila inaelezwa kuwa alikuwa ni mpwa aliyependwa zaidi na mke wa zamani wa Hulk, huku wadada hao wawili wakiwa wamewahi kutuma picha zao kwenye Instagram, wakifurahia maisha.

 

Camila alituma ujumbe mrefu kwa Iran kwenye Instagram akimueleza kuhusu penzi lake na Hulk.

Camila aliandika: “Shangazi Iran, kwanza nataka nikuambie kuwa ujumbe huu siyo wa kujieleza au kujisafisha.

 

“Nakupenda sana na kukujali, ndiyo maana naongea hapa. Nataka ujue vitu ambavyo pengine kila mtu ataongea tofauti, lakini siwahukumu kwa kuwa watu wa nje huwa hawajui chochote na wengi wao wanataka mambo yawe mabaya.

 

“Sikutarajia kama inaweza kutokea, lakini hatuwezi kupuuza matakwa ya moyo, hakuna mtu ambaye anaweza kupuuza moyo wake.

“Samahani kwa kila kitu. (Hulk) alinionyesha kuwa hakukuwa na uwezekano wowote wa ninyi kurudiana, kwa hiyo tukajiruhusu kuishi kwa matakwa ya mioyo yetu.”

 

Iran alionekana kukasirishwa na uhusiano mpya wa ndugu yake huyo na mumewe wa zamani.

Iran alisema: “Moyo wangu unajuta kwamba ndugu Hulk, akiwa hajaridhika na kuisitisha ndoa ya miaka 12, ameonyesha kutoheshimu maumivu ya mtu ambaye siku zote alimuonyesha upendo, heshima na kuwalea watoto wake.”

 

Hulk ana watoto watatu na Iran, Ian mwenye miaka 10, tiago (8) na Alice (6).

Nyota huyo wa zamani wa Porto na Zenit Saint Petersburg, kwa sasa anaogelea mshahara mnono wa pauni 320,000 (Sh mil 957) kwa wiki China.

RIO DE JANEIRO, Brazil

Leave A Reply