The House of Favourite Newspapers

Humud azungumzia mustakabali wake

KUELEKEA usajili wa dirisha, kiungo aliyeachana na KMC hivi karibuni, Abdulhalim Humud, ameizungumzia hatma yake baada ya kuachana na timu hiyo.

 

Humud ambaye aliwahi kuichezea Simba na Azam kwa nyakati tofauti, hivi karibuni alivunjiwa mkataba wake na KMC kutokana na utovu wa nidhamu.

Akizungumza na Championi Jumatano, Humud alisema kwa sasa anaendelea kujifua vikali ili kujiweka fiti kabla ya kuona mustakabali wake utakuwaje.

 

“Nipo bize na kipindi hiki nafanya mazoezi kwa ajili ya kujiweka fiti, sitaki kukumbuka yaliyopita, kikubwa nahitaji kuona nafanyaje siku zijazo.

“Nipo tayari kujiunga na timu yoyote kipindi hiki cha usajili na tayari kuna timu kadhaa zimeanza kunifuatilia,” alisema Humud.

 

Ikumbukwe kuwa, dirisha dogo la usajili linalotarajiwa kufunguliwa kesho Alhamisi, litafungwa Desemba 15, mwaka huu ambapo timu za Ligi Kuu Bara, ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili zitapata fursa ya kusajili.

 Isaya Mbena, Dar es Salaam

Vigogo Yanga Wapigwa ‘Stop’ Miaka 3 kujihusisha na soka, wapigwa faini

Comments are closed.