Husna Maulid Afanya Manjonjo Msibani

Husna Maulid.

MUUZA nyago wa video za wasanii mbalimbali za wanamuziki Bongo, Husna Maulid mwishoni mwa wiki iliyopita alitinga kivazi kilichozua mjadala kwenye msiba wa video queen mwenzake Agness Gerald Masogange’ huku akifanya ‘manjonjo’ ya kucheza na kulamba Ice cream.

 

Akizungumza na Gazeti la Amani, Husna alisema hakuwa na huzuni sana msibani hapo kama wengine waliolia sana, kwani kikubwa anachokiangalia yeye ni kuyaenzi yale mazuri aliyoyafanya Masogan “Acha mimi nimuenzi Masogange kwa kufuata yale mazuri na siyo kulia sana hapa msibani ndiyo maana naweza nikacheza kidogo kama hivi huku nikila zangu Ice cream,” alisema Husna.

Stori: Imelda Mtema.


Loading...

Toa comment