The House of Favourite Newspapers

Shamsa Ford Acharuka Mastaa Kuibiana Mabwana

 

Shamsa Ford

MSANII anayefanya vizuri Bongo Muvi, Shamsa Ford amefunguka kuwa hakuna kitu anachokiheshimu kama mwanaume wa mtu wake wa karibu lakini anashangaa wasanii wengi wamekuwa wakiiba wanaume wa watu.

 

Akizungumza na Amani bila kuwataja majina, Shamsa alisema kuna baadhi ya mastaa wanajua wazi mwanaume anayemtongoza ni wa rafiki yake lakini akijua tu ana fedha yuko radhi hata ajifanye kama hamjui huyo rafiki yake ili mradi tu atembee naye.

 

“Mimi jamani niko tofauti kabisa siwezi mwanaume wa rafiki yangu akanitongoza nikakubali ninaheshimu hilo lakini wengine wako radhi wakukane ili mradi tu apate fedha,” alisema Shamsa huku akibainisha kuwa hakuna mwanamke atakayemsogelea mumewe Chidi Mapenzi kwani ni mwaminifu na hawezi kumsaliti.

Stori: Imelda Mtema.

Comments are closed.