The House of Favourite Newspapers

Huyu Mnigeria Mpya wa Simba ni Noma!

0

INAELEZWA kuwa mabosi wa Simba wamemwaga dola 70,000, ambazo ni sawa na Sh milioni 162 za Kitanzania, kukamilisha usajili wa mshambuliaji wao mpya, Junior Lokosa, mwamba wa Nigeria.

 

Chanzo makini kutoka ndani ya Simba kimesema kuwa uzoefu wa mchezaji huyo kwenye michezo ya kimataifa na kupita kwenye timu kubwa za Nigeria na Esperance ya Tunisia, inatajwa kuwapa jeuri viongozi wake ambao hawakutaka auzwe chini ya dola 100,000.

 

Hata hivyo, baada ya mazungumzo na Simba, menejimenti ya mchezaji huyo ikakubali kulegeza kitita hicho na akamwaga wino Msimbazi kwa dola 70,000 kwa mkataba wa miezi sita, ukiwa na kipengele cha kumuongezea miaka mingine miwili kama ataonyesha uwezo.

Nyota huyu alitakiwa kufanya majaribio Zanzibar kwenye Kombe la Mapinduzi lakini akachomoa akiamini uwezo wake, ndipo Simba wakaamua kumpa mkataba wa miezi sita ili wamtazame kwanza.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu,mtoa taarifa wetu kutoka ndani ya Simba, alisema: “Lokosa amepewa dola 70,000 kama sehemu yake ya usajili, huku mshahara wake pia ukitajwa kufi kia dola 8,000 (zaidi ya Sh milioni 18). Walikuwa wanavutana kati ya viongozi wa Simba na menejimenti ya mchezaji huyo ambaye hawakutaka asaini chini ya dola 100,000 (Sh milioni 231).

 

”Lokosa, mwenye umri wa miaka 27, ni mshambuliaji wa kati mwenye uwezo mzuri wa kufunga mabao, amewahi kuzitumikia klabu za First Bank na Kano Pillars, zote za Nigeria, kisha akajiunga na Esperance ya Tunisia 2019 na kudumu hadi Juni 2020.

 

Bado hajatambulishwa na Simba lakini ndiyo tayari ameshamwaga wino Msimbazi na mambo yakienda sawa anaweza kutangazwa muda wowote kuanzia sasa.Alipotafutwa Afi sa Mkuu wa Uendeshaji wa Simba Sports Club Ltd, Dk Arnold Kashembe ili azungumzie ishu hiyo, alisema:

 

“Mimi siwezi kuzungumzia suala hilo, kwa sababu lipo nje ya uwezo wangu, Simba kuna mgawanyiko wa majukumu, hivyo hata kama kweli au siyo kweli siwezi kuthibitisha, mtafute meneja au C.E.0.”Meneja wa Simba Abbas Ally na Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez, walipotafutwa simu zao zilikuwa zinaita bila kupokelewa licha ya kupigiwa zaidi ya mara moja.

 

Lukosa wakati akiwa anaitumikia Kano Pillars ya kwao Nigeria alifanikiwa kufunga mabao 19 akizidiwa na Mfon Udoh aliyefunga mabao 23 na Jude Aneke (mabao 20) msimu wa 2018-19.

 

Katika msimu huo, alifanikiwa kushinda tuzo ya mfungaji bora ndani ya kikosi cha Kano Pillars baada ya kufunga mabao 19 katika mechi zaidi ya 20. Lakini mshambuliaji huyo mwaka jana aliondoka Kano Pillars na kujiunga na Esperance Tunis ambapo katika kipindi cha mwaka mmoja na miezi saba alifanikiwa kucheza mechi 11.

 

Katika mechi hizo za kimashindano, Lukosa alicheza mechi sita za Ligi Kuu ya Tunisia ambapo alifanikiwa kufunga bao lake moja huku akifanikiwa kucheza mechi nne pekee za Ligi ya Mabingwa Afrika bila kufunga bao lolote.Kwa upande wa Kombe la Tunisia, mshambuliaji huyo raia wa Nigeria alifanikiwa kucheza mechi moja pekee huku akikosa michuano ya FA ya nchi hiyo kutokana na majeraha ya goti yaliyokuwa yakimsumbua.

 

Kwa upande wa makombe mshambuliaji huyo amefanikiwa kushinda ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa na Esperance katika msimu wa 2018-19 pamoja ya ubingwa wa Ligi ya Tunisia.Katika mwaka 2019 ameshinda ubingwa wa Kombe la Tunisia na ubingwa wa Kombe la FA kabla ya Juni, mwaka jana kuachana na timu hiyo.Simba imemchukua nyota huyu maalum kwa ajili ya mechi za kimataifa.

Leave A Reply