The House of Favourite Newspapers

HUYU NDIYE MASOGANGE TUNAYEMJUA

KIFO cha ghafla cha mwa­namitindo au Video Queen wa Bongo Fleva, Agness Ger­ald almaarufu Masogange, kimeibua mshtuko mkubwa.

Jana, jioni, gazeti hili lilipokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Masogange kilichotokea kwenye Hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge jijini Dar.

 

Akithibitisha kutokea kwa kifo hicho, Afisa Habari wa Chama cha Waigizaji wa Wilaya ya Kinondoni, Dar, Masoud Kaftany aliliambia gazeti hili kuwa, kifo hicho kilijiri majira ya saa 10:30 jioni ambapo mwili wake ulipelekwa katika Hospitali ya Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.

“Ni kweli na mimi nimepata taarifa hizo na amepelekwa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi,” alithibitisha Kaftany.

Taarifa za awali zilizopatikana hospi­talini hapo mara tu baada ya kifo hicho zilieleza kwamba, Masogange alikuwa akisumbuliwa na Ugonjwa wa Homa ya Tumbo (Typhoid Fever) na Upungu­fu wa Damu Mwilini (Anaemia).

 

MASOGANGE NI NANI?

Kabla ya kukutwa na umauti, mtu alipokuwa akizungumzia warembo wa­zuri ndani ya Jiji la Dar ni wazi kwamba asingeacha kulitaja jina la Masogange.

Jina la Masogange lilikuwa kubwa mno kutokana na kujishughulisha na upambaji wa video za wasanii mbalim­bali wa Bongo Fleva.

Kumbukumbu kwenye makabrasha ya gazeti hili zinaonesha kuwa, Ma­sogange alizaliwa Aprili 23, 1988 kwenye Hospitali ya Mkoa wa Mbeya. Masogange alisoma katika shule ya Msingi na Sekondari ya Sangu jijini Mbeya kabla ya kuendelea na kidato cha tano na sita na baadaye alitinga jijini Dar katika harakati za kutafuta maisha.

Aliingia katika kazi ya uanamitindo kupitia video za wanamuziki mbalim­bali kutokana na umbo lake matata lil­ionekana kuwa na mvuto kwenye video hizo.

Masogange ametokea katika fa­milia ya wacha Mungu na kwamba wazazi wake hawakuafikiana naye katika kujishughulisha na kazi ya kuuza sura katika video za wasanii wa muziki wa kidunia.

Katika mahojiano mbalimbali na Magazeti ya Global, Masogange alieleza kuwa ana shughuli zake binaf­si ambazo zilikuwa zikimuingizia fedha kumudu kuendesha maisha yake. Wen­gi hawajui, lakini Masogange ameacha mtoto mmoja wa kike.

 

Masogange alianza kuvuma zaidi baada ya kuonekana kwenye video ya Wimbo wa Masogange wa msanii ku­toka Morogoro, Abednego Damian al­maarufu Belle 9 kisha alitumbulia kwe­nye Bongo Movies.

Jina lake lilizidi kuwa maarufu pale alipohu­sishwa na skendo ya usafirishaji wa dawa za kulevya aina ya Crystal Metham­phetamine am­bapo alikamat­wa nchini Afrika Kusini na baadaye ma­hakama nchini humo ilikanu­sha kuwa dawa hizo hazikuwa za kulevya bali za matumizi ya kimaabara kwa ajili ya tiba za kibi­nadamu.

 

Ukiacha msala huo wa Af­rika Kusini, mwaka jana, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda al­imtaja kwe­nye orodha ya mastaa wanaotumia madawa ya kulevya hivyo kushikiliwa na kesi yake kuun­guruma katika Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu, Dar.

Katika kesi hiyo, Aprili 3, mwaka huu, Ma­sogange alihu­kumiwa kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya shilingi milioni 1.5 kwa kosa la kutumia kutumia madawa ya kulevya aina ya Heroin na Oxazepam ambapo alikubali kulipa faini hiyo hivyo aliach­iwa huru. Tangu hapo, Masogange hakuone­kana tena hadi kuibu­ka kwa mshtuko wa kifo chake.

 

Global Group tu­naungana na familia, ndugu, jamaa na marafi­ki wa Masogange katika kipindi hiki kigumu. Rest In Peace Masogange!

Mbali na Video ya Wim­bo wa Masogange, video nyingine alizoonekana Masogange ni Magube­gube ya msanii Barnaba Elias au Barnaba Boy na ile ya msanii Tundaman iitwayo Msambinungwa.

Comments are closed.