The House of Favourite Newspapers

Huzuni! Rais Hussein Mwinyi, Kabla Na Baada ya Kutoa Heshima Za Mwisho Mbele Mwili Wa Baba Yake

0

Wakijiandaa kwenda kutoa heshima za mwisho.                                                                                                                                               Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Hussein Mwinyi, leo alikuwa na wakati mgumu uliojaa huzuni kabla na baada ya kutoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lilikuwa na mwili wa marehemu baba yake aliyekuwa Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania Awamu Ya Pili.

Rais wa Zanzibar, Hussein Mwinyi na mkewe wakitoka kutoa heshima za mwisho.

Katika tukio hilo lililojaa huzuni kubwa, Rais Hussein akiwa ameambatana na mkewe walionekana kuingia na sehemu maalum yenye kibanda cha kutolea heshima za mwisho na kutoka huku wakionekana na nyuso zilizojaa huzuni.

Rais Hussein Mwinyi wakiwa na huzuni baada ya kutoa heshima za mwisho.

Mwili wa Hayati Ali Hassan Mwinyi aliyeaga dunia jana katika Hospitali ya Mzena jijini Dar unatarajiwa kuzikwa kesho kwao, Kisiwani Zanzibar. Bwana alitoa, Bwana alitwaa, Jina lake lihimidiwe. HABARI/PICHA NA RICHARD BUKOS /GPL

Leave A Reply