The House of Favourite Newspapers

Ibada ya Kanye West na Kim Kardashian, Majirani Wacharuka!

Mwanamuziki wa Marekani Kanye west anaendelea na mpango wake wa kufanya ibada na familia yake kila jumapili Ibada hii hufanyika kwa  burudani kubwa kutoka kwenye bendi yake Kanye West.

Ibada iyo ambayo waumini wake hufika kwa kupewa mualiko sio kila mtu anaweza kwenda. Unaambiwa ukipata mwaliko wa kwenda kwenye ibada iyo unatia saini makubaliano ya kuto kwenda na mtu mwingine ambaye hahusiki katika ibada hiyo. Wasanii ambao wamewahi kuhudhuria ibada ya Kanye West ni  DMX, Chance the raper na Kid Cudi.

Mke wa Kanye, Kim Kardashian amekuwa akitumia mitandao yake ya kijamii ku-post baadhi ya picha za video kuonyesha yaliyojiri wakati wa ibada mara nyingi  majirani zake kanye wamekuwa wakilalamika juu ya ibada hizo anazofanya kwa kupiga kelele za mziki mkubwa nyumbani kwake au maeneo ya mlimani jirani na nyumbani kwakwe kila Jumapili.

Comments are closed.