Ibrahim Ajibu Aingia Anga za Al Ahl

KIUNGO mshambuliaji mpya wa Simba, Ibrahim Ajibu, amekiangalia kikosi cha timu yake na kutamka kuwa hawana sababu ya kuukosa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwani wao ni matawi ya juu sana.

 

Kiungo huyo amepata nafuu ya majeraha ya goti aliyoyapata hivi karibuni akiwa kwenye kikosi cha Taifa Stars inayowania kufuzu kucheza Chan. Akizungumza na Spoti Xtra, Ajibu alisema kuwa wana kikosi imara na bora cha kutwaa ubingwa huo wa Afrika na lengo ni kuzifikia rekodi za klabu kubwa za Zamalek, Al Ahly na TP Mazembe.

 

Ajibu alisema kuwa kama walifanikiwa kufika hatua ya robo fainali ya mashindano hayo kabla ya kuondolewa TP Mazembe ya Kinshasa nchini DR Congo, basi hakuna kitakachoshindikana kwao msimu huu.

Aliongeza kikosi chao kimeboresha msimu huu kwa kusajili wachezaji wenye sifa, uwezo na uzoefu wa michuano hiyo, hivyo hana hofu huku akiwataka mashabiki kuendelea kujitokeza uwanjani watakapocheza kwa ajili ya kuwasapoti.

 

“Nimefanya mazoezi na kucheza baadhi ya michezo ya kirafiki ya kimataifa na timu yetu kupata matokeo mazuri tukiwa kambini Sauzi na baadaye kurejea nyumbani jijini Dar es Salaam.

 

“Nikiwa nacheza michezo hiyo ya kirafiki nimegundua kuwa tuna kikosi imara kitakacholeta ushindani wa michuano hii mikubwa ya Afrika ikiwemo kuchukua ubingwa na hilo ndiyo lengo letu kwa kuanzia sisi wachezaji, benchi la ufundi na viongozi.

 

“Timu inacheza kwa nidhamu ya hali ya juu ikiwemo kulinda goli na kushambulia ndani ya wakati mmoja, hivyo ni matarajio yangu kuona timu ikiendelea kufanya vema zaidi,” alisema Ajibu ambaye meneja wake ni kaka yake.


Loading...

Toa comment