The House of Favourite Newspapers

Idris Sultan, Alamba Shavu la Ubalozi Kampeni ya Uhamasishaji ya M-Pesa Imeitika

0
Mkuu wa Idara, maendeleo ya biashara M-Pesa, Tulisindo Mlupilo akimuwekea mafuta dereva wa bodaboda, Alli Juma eneo la Manzese wakati wa uzinduzi wa kampeni ya M-Pesa Imeitika ikihusisha huduma ya Wese activation ambapo madereva 125 wa boda boda walipata ofa ya kuwekewa mafuta bure wanapolipa kwa M-Pesa, Kampeni hii Itawazawadia wateja wa M-Pesa kila wanapotumia huduma za kidigitali za M-Pesa. Wengine wapili kulia ni Mkurugenzi wa Udhibiti wa Hatari na Utii wa sheria Vodacom Tanzania Plc, Agapinus Tax na kulia ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Digitali na huduma za ziada wa kampuni hiyo Nguvu Kamando.

 

 

Dar es Salaam, 6 Julai 2022. Vodacom Tanzania, kampuni ya huduma za teknolojia na mawasiliano inayoongoza, leo imezindua kampeni inayoitwa ‘M-PESA IMEITIKA’  ambapo msanii, Idris Sultan ndiye aliyelamba shavu la ubalozi wa kampeni hiyo.

 

Lengo la kampeni ni kuhimiza matumizi ya kidijitali ya M-pesa kwenye shughuli za bima, afya, mikopo, kutuma na kupokea pesa nje ya nchi.

Mkurugenzi wa Udhibiti wa Hatari na Utii wa sheria Vodacom Tanzania Plc, Agapinus Tax akimuwekea mafuta dereva wa bodaboda wakati wa uzinduzi wa kampeni ya M-Pesa Imeitika ikihusisha huduma ya Wese activation ambapo madereva 125 wa boda boda walipata ofa ya kuwekewa mafuta bure wanapolipa kwa M-Pesa, Kampeni hii Itawazawadia wateja wa Vodacom kila wanapotumia huduma za kidigitali za M-Pesa. Wengine kulia ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Digitali na huduma za ziada wa kampuni hiyo Nguvu Kamando na Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Olaf Mumburi.

 

 

Akizungumza wakati wa uzinduzi, mkuu wa idara ya maendeleo ya biashara na masoko wa Vodacom Tanzania, Tulisindo Mlupilo alisema,

 

“Tuna mtazamo wa kuongoza Tanzania kuelekea katika zama za kidijitali na kubadilisha maisha kwa kutumia teknolojia kupitia uchumi wa kidijitali pamoja na ushushwaji wa tozo ili kuhakikisha Watanzania wote wanapata huduma za kidijitali.”

Kampeniya M-PESA IMEITIKA itakuwa ikitoa zawadi za kila siku, kila wiki, pamoja na zawadi nono itakayotolewa kwa wale wateja ambao watachukua fursa ya tozo mpya ya huduma iliyopunguzwa kwa kutumia huduma za M-Pesa pamoja na kutumia huduma zingine za M-Pesa kama Vodabima, M-Pesa Visa card na mengine mengi.

Mkuu wa Idara ya M-Pesa Biashara, Happiness Shuma akimuwekea mafuta dereva wa bodaboda, Abdrahaman Bakari eneo la Manzese wakati wa uzinduzi wa kampeni ya M-Pesa Imeitika pamoja na zawadi nyingine ikihusisha huduma ya Wese activation ambapo madereva 125 wa bodaboda walipata ofa ya kuwekewa mafuta bure baada ya kulipa kwa M-Pesa, Kampeni hii Itawazawadia wateja wa Vodacom kila wanapotumia huduma za kidijitali za M-Pesa. Wengine ni Mkurugenzi wa Udhibiti wa Hatari na Utii wa sheria Agapinus Tax (wa tatu kulia) na Mkurugenzi wa Kitengo cha Digitali na huduma za ziada wa kampuni hiyo Nguvu Kamando (wa pili kulia) pamoja na Balozi wa M-Pesa Imeitika , Idriss Sultan.

 

 

“Watumiaji wa huduma za kidijitaliza M-Pesa kama vile kutuma pesa ndani na nje ya nchi, kufanya malipo watapata nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali.

 

Zawadi hizo ni pamoja na bajaji na bodaboda, kujaziwa mafuta ya gari, miezi mitatu ya bima ya   ajali, na mwisho wa kampeni kutakuwa na zawadi kuu ambayo ni nyumba mpya iliyojengwa jijini Dar es Salaam yenye thamani ya Shilingimilioni 100.”

 

Mfumo wa M-PESA wa Vodacom Tanzania umekuwa ukiongoza kwa ubunifu tangu kuzinduliwa kwake mwaka 2008. Katika muda huu, mfumo umeongoza kwa kutoa huduma za kutuma na kupokea pesa kutokana na urahisi wa matumizi pamoja na usalama wake. M-PESA imekuwa maarufu kwa matumizi na mahitaji ya malipo ya kibiashara.

 

Vodacom imejitahidi kuongeza huduma mpya zinazopatikana kupitia mfumo wa M-PESA na sasa watumiaji wanaweza kupata mikopo midogomidogo kupitia SONGESHA na M-PAWA. Vikundi vya kijamii vinatumia huduma ya M-KOBA kutimiza malengo yao.

 

Kampeni ilizinduliwa na moja ya vivutio vya kampeni, ‘WESE’. Kupitia shindano la ‘WESE’, madereva watakaonunua aina yoyote ya bima kupitia huduma ya  VodaBIMA watapata nafasi ya kushinda mafuta ya petrol au dizeli yenye thamani ya Shlingi 20,000 kwenye vituo vinavyoshirikiana vile vile washindi 10 watabahatika kujaziwa tenki.

 

Ili kushiriki, watumiaji wanahitaji kufanya muamala wowote kupitia M-PESA, kuanzia kutuma pesa hadi kufanya malipo ya serikali au kulipia huduma kama za VodaBIMA. Piga Namba*150*00#, kisha chagua muamala wowote wa M-Pesa au kwa urahisi zaidi tumia M-Pesa App.

 

Kuhusu Vodacom Tanzania M-Pesa

Vodacom M-Pesa ndiyo inayoongoza nchini kwautoaji wa huduma za kifedha kupitia mtandao. Huduma ilizinduliwa na Vodacom Tanzania Plc mwaka 2008.

 

Ikiwa sasa imethibitishwa na GSMA na kuwa na watumiaji zaidi ya milioni 10, M-Pesa imekuza kwa kiasi kikubwa ushirikishwaji kifedha na shughuli za kiuchumi nchini. Wateja wanaweka na kutoa pesa kwenye akaunti zao za M-Pesa kupitia mtandao wa mawakala zaidi ya 108,000 nchi nzima.

 

Mfumo wa M-Pesa unaunganisha biashara, mabenki na taasisi za serikali na hivyo kuwezesha miamala kidijitali. M-Pesa inendelea kuongoza katika utoaji wa huduma bunifu zinazoboresha na kurahisisha Maisha ya watumiaji wake.

Leave A Reply