The House of Favourite Newspapers

Ifahamu Historia Ya Msanii Justin Bieber

0
Mwanamuziki Justin Bieber.

Justin Bieber alizaliwa Machi Mosi,  1994, Ontario nchini Canada. Mama yake anaitwa Pattie Mallete na baba yake ni Jeremy Bieber.

Mwanamuziki huyo amezaliwa kwenye familia ya watoto watatu na ana wadogo zake wawili,  Jaxon na Jazmyn.

Harakati zake za muziki zilianzia mtaani ambapo alikuwa anafanya shoo  kwenye matamasha na alifanikiwa kuingiza kipato kidogo kupitia matamasha hayo akiwa mdogo.

Kuna kipindi alihitaji kufanya kazi na Kampuni ya Simu ya Blackberry tena bure kabisa lakini kampuni hiyo ilimkatalia na ndipo alipoamua kufanya ngoma zake kivyake huku akimsikilizisha mama yake.

Akiwa na umri wa miaka 13 ndipo mama yake akaanza kuamini kipaji chake na kuamua kuposti katika Mtandao wa Kijamii wa Youtube kipande cha video kikimuonyesha Bieber akiimba huku akipiga gitaa.

Video hiyo ilisambaa sehemu mbalimbali na ikafungua nuru ya mafanikio kwa Bieber na hii ni baada ya meneja mmoja, Scooter Braun kuiona video hiyo akaipenda na kuamua  kumtafuta na kumpeleka katika Studio ya Atlanta kwa ajili ya kurekodi demo.

Na kwa mara ya kwanza akakutana na msanii Usher Raymond ambaye alimsaidia kwa kiasi kikubwa mpaka akafanikiwa kuachia ngoma yake ya kwanza mwaka 2008 na mwaka 2010 akaachia album yake inayoitwa My World 2.0, hivyo kujizolea  mashabiki wengi kupitia nyimbo zake kama vile Sorry, Love Yourself, Love Me , What Do You Mean na nyingine nyingi.

Lakini pia ameshafanya collabo na wasanii wakubwa wa Marekani akiwemo Chris Brown kwenye wimbo uitwao Next to You.

Mwaka 2010 aliachia ngoma ya Never Say Never aliyomshirikisha Jaden Smith, kutokana na ujumbe mzuri uliopo kwenye wimbo huo ambao unawahamasisha watu kutokata tamaa, ulisababisha baba yake Jaden ambaye ni muandaaji na mchezaji maarufu wa filamu nchini Marekani,  Will Smith kuandaa filamu aliyoipa jina la Karate Kid huku mchezaji mkuu akiwa ni Jaden filamu akishirikiana na Jackie Chan filamu ambayo ilipata umaarufu mkubwa na kufanya vizuri kwenye mauzo sokoni.

Uzuri wa wimbo wenyewe na filamu hiyo ulimfanya Bieber kushinda tuzo za kimataifa ikiwemo ya Grammy, MTV MAMA,  Billiboard, Kids Choice, Teens na nyingine nyingi.

Baada ya kupata tuzo hizo jina la Bieber lilizidi kuwa kubwa, akafahamika duniani kote hali iliyomvimbisha kichwa na akaanza kufanya vituko.

Aliwahi kuingia kwenye nyumba ya jirani yake akachukua ndoo na kuikojolea , pia aliwahi kumpiga mwandishi wa habari  wa Miami na matukio mengi.

Bieber alikuwa  na uhusiano wa kimapenzi kwa muda mrefu na msanii mwenzake Selena Gomes na baadaye ukavunjika ikasemekana kuwa anatoka kimapenzi na wasichana tofauti akiwemo Sophia Richie, Hailey Baldwin na wengine wengi.

(Stori: Isri Mohammedi/GPL)

Leave A Reply