The House of Favourite Newspapers

Igangula: Miezi mitatu tu, Yanga Ina Uwanja Wake

Mbaraka Igangula

MGOMBEA wa nafasi ya mwenyekiti ndani ya Klabu ya Yanga, Mbaraka Igangula, amesema ndani ya mwezi mmoja, atahakikisha Yanga inafanya usajili wa maana.

 

Mbali na kufanya usajili wa maana, pia kwa kipindi cha miezi mitatu ya uongozi wake ndani ya klabu hiyo, uwanja wa mazoezi kwa ajili ya timu utakuwa umepatikana. Igangula ametoa ahadi hizo wakati akifungua kampeni zake jijini Dar es Salaam jana Jumanne kuelekea uchaguzi mkuu wa klabu hiyo unaotarajiwa kufanyika Jumapili hii.

Jumapili hii ya Mei 5, Wanachama wa Klabu ya Yanga watafanya uchaguzi mkuu wa kumchagua mwenyekiti, makamu mwenyekiti na wajumbe ambao wataiongoza klabu hiyo kwa kipindi kijacho cha miaka minne baada ya viongozi woe wa awali wakiongozwa na mwenyekiti, Yusuf Manji kujiuzulu.

 

“Nikipata ridhaa ya kuwa mwenyekiti ndani ya Yanga, nitahakikisha ndani ya mwezi mmoja unafanyika usajili makini kwa ajili ya timu yetu ambayo msimu ujao tunataka ifanye vizuri kwenye mashindano yote tutakayoshiriki na kurudisha ile hadhi ya Yanga iliyopotea.

 

“Pia suala la uwanja wa mazoezi kwa ajili ya timu yetu, hilo litatimia ndani ya miezi mitatu kwani tayari kuna watu wamejitokeza kuhakikisha hilo tunalifanikisha.

 

“Mbali na hayo, nitasimamia utengenezaji wa hosteli ambazo hapo zitakaa timu zetu zote kuanzia ile ya vijana, wanawake na ile timu kubwa ya wanaume. Itakuwa na kila kitu.”

 

Alisema Igangula. Katika hatua nyingine, Igangula alisema anamiliki ghorofa zaidi ya tano, hivyo akiingia madarakani moja atalikabidhi kwa Yanga kufanyia shughuli zake za kimaendeleo.

 

“Nataka kuondoa ufisadi ndani ya Yanga, huo ufisadi ndiyo umetufikisha hapa mpaka leo tunatembeza bakuli, nikiingia madakarani, nembo ya Yanga itaheshimika na kuwa sehemu kubwa ya kutuingizia mapato,” alimaliza Igangula hook akisisitiza kuwa ile kauli mbiu yake ya Umoja na Mshikamano, ndiyo silaha ya ushindi kwake.

Comments are closed.