The House of Favourite Newspapers

JPM: NIONGEZE MSHAHARA? BADO SIJAONDOKA MADARAKANI! – VIDEO

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai, Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe Jenista Mhagama na viongozi wa Wafanyakazi wakishikana mikono na kuimba wimbo wa MSHIKAMANO (Solidarity Forever) wakati wa sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani maarufu kama Mei Mosi katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya leo Jumatano Mei 1. 2019

Kila mwaka tarehe Mosi Mei, Dunia huadhimisha siku ya wafanyakazi ambapo kwa mwaka huu sherehe hizo Kitaifa zimefanyika mkoani mbeya na mgeni Rasmi akiwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli.

 

Wafanyakazi walikuwa na shauku kubwa ya kusikia Mhe. Rais akitangaza kauli ya kupandisha mishahara yao lakini wakati akijibu hotuba ya Chama cha Wafanyakazi (TUCTA), Rais Magufuli amesema alishaahidi ataongeza mshahara kabla ya kumaliza muda wake hivyo watumishi waw wavumilivu atawaongezea tu.

Ris wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa cheti cha mfanyakazi bora Mkuu wa TEHAMA wa Wizara ya Fedha Bw. John Sausi wakati wa Sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya Leo Jumatano Mei 1, 2019

“Katibu Mkuu wa TUCTA amenikumbusha ahadi yangu ya mwaka jana kuwa kabla sijaondoka madarakani nitaongeza mishahara. Lakini lazima tuelewe kuwa bado sijaondoka madarakani na kwa maelezo niliyoyatoa inaonesha uchumi unakua. Subira yavuta heri

“Kuna bango moja limeandikwa “Tupandishe Madaraja nasi tupande Bombardier”. Kuanzia mwaka 2015 tumewapandisha madaraja zaidi ya watumishi laki 1 na 18 elfu. Pia tumelipa madai yasiyo ya mishahara na mengi yalikuwepo kwa zaidi ya miaka 10.

“Ningeweza kuwaongezea elfu 5 au 10, kesho tu bidhaa zingeanza kupanda hivyo lazima kwanza tujenge uchumi imara. Mimi mwenyewe nilikuwa mwalimu na nikaenda kuoa mwalimu anayejua shida zetu Serikali inawapenda wafanyakazi.

 

“Maendeleo yetu hapa nchini ni matokeo ya kufanya kazi kwa bidii, mchango wa wafanyakazi ni mkubwa katika kuchangia uchumi wa nchi, hongereni sana wafanyakazi. Sasa hivi kila mwezi tunatumia takribani bilioni 580 kulipa mishahara na huwa tunaanza kulipa kuanzia tarehe 19. Lakini pia tunatumia fedha nyingi kulipa madeni hivyo mnaweza kuona kiasi gani kinabaki kwa miradi ya maendeleo.

 

“Baadhi ya mapendekezo yenu tumeanza kuyatendea kazi ikiwemo kufufua shirika la uvuvi na kujenga meli mpya ziwa Nyasa na Victoria.Yote haya tunafanya kwa kushirikiana na watu wa Japan Ili kuwavutia watalii tumeanza kutanua viwanja 11 na kununua ndege 8. Natoa wito kwa waajiri kusimamia Sheria za Kazi ikiwemo usalama katika sehemu za kazi. Vilevile wahakikishe wafanyakazi wao wana mikataba,” amesema Magufuli.

 

Maadhimisho hayo yamebebwa na kauli mbiu ya ”Tanzania ya Uchumi wa Viwanda Inawezekana, Wakati wa Mishahara na Maslahi Bora ni Sasa.”

 

SIKILIZA HOTUBA YA MAGUFULI HAPA

Comments are closed.