The House of Favourite Newspapers

IGP Afanya Mabadiliko Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Songwe na Rukwa 

0

IGP Camillus Wambura amemhamisha aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Fortunatus Muslim kwenda kitengo cha miopango makao makuu na nafasi yake imechukuliwa na ACP Alex Mukama ambaye alikuwa RPC Songwe.

Taarifa hiyo imetolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi SACP David Misime, na kwamba IGP pia amemhamisha aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa ACP Theopista Mallya, kwenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe

IGP Wambura pia amemhamisha ACP Shedrack Masija ambaye alikuwa Afisa Mnadhimu Namba Moja mkoa wa Simiyu, kwenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa

KWA MARA ya KWANZA FEISAL AZUNGUMZA BAADA ya KUTOKA TFF – “NIPO SAWA TU”…

Leave A Reply