The House of Favourite Newspapers
gunners X

IGP Sirro: Wananchi wa Kibiti na Ikwiriri Wajilinde (VIDEO)

0

 

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amewataka wakazi wa maeneo ya Ikwiriri na Kibiti mkoani Pwani pamoja na maeneo mengine, wachukue jukumu la kujilinda kupitia vikundi vya ulinzi shirikishi, kutokana na asili ya maeneo yao kutofikiwa kwa urahisi na pikipiki za polisi.

IGP Sirro ameyasema hayo mapema leo kwenye Bwalo wa Polisi Oysterbay (Police Officers’ Mess) jijini Dar, wakati akipokea msaada wa magari ya kuboresha mapambano dhidi ya uhalifu, kutoka kwa Kampuni ya Great Wall Motors and Haval kutoka nchini China ikiwa ni sehemu ya kudumisha uhusiano bora wa Kidemokrasia uliopo baina ya nchi hiyo na Tanzania.

“Suala la kudumisha vikundi vya ulinzi shirikishi ni la muhimu sana, hususan kwa maeneo ya Ikwiriri na Kibiti, ambako wananchi ni lazima wajilinde, kwa sababu kuna baadhi ya maeneo ambayo pikipiki za polisi hazifiki lakini si Kibiti na Ikwiriri tu, hata maeneo mengine , mfano mikoa ya Lindi na Mtwara na nchi nzima.

“Nigusie kidogo kuhusu Kibiti na Ikwiriri, ingawa mimi si mtu wa kusema sana, lakini tunaendelea vizuri na muda si mrefu mtapata majibu, nishukuru sana kwa ushirikiano wa wananchi wa Kibiti na Ikwiriri kwa ushirikiano wao, Tanzania haijazoea mambo ya kihalifu, sasa kama walidhani ni rahisi, walitumwa vibaya na sisi tutawajibu vibaya, ” alisema IGP Sirro na kumalizia;

“Tumepokea msaada wa magari kutoka kwa wenzetu, ikiwa ni sehemu ya kudumisha uhusiano mzuri uliopo, yatasaidia kupambana na uhalifu.”

Leave A Reply