The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Bunge Latii Agizo la JPM

0

IKIWA ni zimekwishapita wiki chache tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli aliombe Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuunda kamati maalum ya kuchunguza mfumo wa uchimbaji wa madini ya Almasi, hatimaye leo bunge hilo limetekeleza agizo hilo.

 

Akitoa tamko rasmi wakati akifunga mkutano wa 7 wa bunge mjini Dodoma leo, Spika wa Bunge, Job Yusto Ndugai amesema ameamua kuunda kamati hiyo maalum, ikiwa ni kutii agizo la Rais Mgufuli, alililotoa wakati wa kupokea ripoti ya kamati maalum ya pili ya sheria ya uchunguzi, iliyoongozwa na Prof. Osolo ikulu jijini Dar, ambapo spika alihudhuria.

 

“Waheshimiwa wabunge, nimeamua kuunda tume maalum itakayochunguza mfumo mzima wa uchimbaji, umiliki na udhibiti wa Madini ya Almasi, ikiwa ni agizo la mheshimiwa rais, kama mtakumbuka nilihudhuria hafla ya kupokea ripoti ya pili na rais akaniomba niunde tume hii na mimi nimefanya hivyo.

 

“Kamati hii, itakuja na mapendekezo maalum baada ya kazi yao, juu ya kuishauri serikali namna bora ya uendeshaji wa shughuli za uchimbaji wa madini hayo,” alisema Spika Ndugai.  

Leave A Reply