Ijumaa Sexiest Girl 2019 Linaanza!  

IJUMAA Lile shindano baab’kubwa la kumtafuta Mrembo wa Gazeti la Ijumaa mwenye mvuto zaidi wa kimahaba (Ijumaa Sexiest Girl), linaanza tena kwa msimu wa mwaka 2019.

Mratibu wa shindano hilo ambaye ni Mhariri wa Gazeti la Ijumaa, Paul Sifael amesema tayari kila kitu kipo kwenye mipango.

“Kifuatacho ni wewe msomaji au shabiki kupendekeza majina ya mastaa wa kike warembo wanaostahili kuingia kwenye kinyang’anyiro hiki ambapo vigezo na masharti lazima vizingatiwe,” alisema Sifael na kuongeza;

“Vigezo na masharti ni pamoja na mrembo au staa husika asiwe ameolewa wala kuwa na mtoto.”

Mapendekezo yanapaswa kuwa na majina ya warembo 20 ambayo yataanza kuchujwa kuelekea kwenye fainali.

“Shindano hili litadumu kwa miezi mitatu hivyo tunakaribisha wadhamini mbalimbali ambao hawatajuta kudhamini kinyang’anyiro hiki,” alisema Paul.

Taji hilo linashikiliwa na mrembo Asha Salum ‘Kidoa’ ambaye alilichukua kutoka kwa Wema Isaac Sepetu.

Unaweza kupendekeza majina ya warembo au mastaa watakaoingia kwenye shindano hili kupitia WhatsApp namba 0684 72 30 43.


Loading...

Toa comment