The House of Favourite Newspapers

Ile Sare ya Stand Utd, Manara Awatoa Hofu Simba

 

OFISA Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara amefunguka na kuwataka mashabiki wa timu hiyo kutohuzunika na matokeo mabaya waliyoyapata dhidi ya Stand United na kudai hicho sio kigezo cha kuharibu katika Ligi Kuu Bara.

 

Manara amesema hayo leo Jumamosi, Machi 03, 2018 wakati akizungumza na wanahabari katika Makao Makuu ya Simba, Kariakoo jijini Dar es Salaam;

 

“Msiangaishwe na matokeo ya mchezo wetu dhidi ya Stand United ‘that is football’ (huo ndiyo mpira wa miguu), kuna vitu hutokea kwa sababu ya mipango ya Mungu, tungeshinda jana ingekuwa nzuri zaidi, lakini kutoa sare kabla ya kuja kucheza na waarabu imekuwa kama ishara kwetu ya kuwa makini katika mchezo huo, Kama tungefunga mabao 5 au 6 mashabiki zetu wangeona mechi na Al Masry kutoka nchini Misri nayo ni rahisi tu,” amesema Manara.

 

Klabu ya Simba itashuka dimbani katika mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Al Masry ya Misri,  Jumatano, Machi 7, 2018 katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam huku viingilio vya mchezo huo vikitajwa kuwa ni VIP A- Tsh 20,000, VIP B- Tsh 15,000 na mzunguko shilingi 5,000.

Comments are closed.