The House of Favourite Newspapers

IMETHIBITISHWA: MEEK MILL, THE GAME WAMALIZA TOFAUTI ZAO

 

Baada ya rapa Meek Mill kumaliza tofauti zake na hasimu wake Drake,muda huu tena amemaliza tofauti kubwa iliyokuwepo kati yake  na rapa The Game baada ya kutoka jela, The Game amethibitisha hilo.

 

Kupitia akaunti yake ya Instagram,  The Game amethibitisha kumaliza tofauti zake na Meek Mill na ilikuwa ni baada ya Meek kutoka jela na kumpigia simu wakaongea kwa muda wa saa moja.

 

Baadhi ya aliyoyaandika yalikuwa:  “Nilikuwa na beef na mwenzangu ambalo lilikuwa ngumu kumalizika, tulikuwa tuna tofauti lakini tumekaa chini na tumekuwa marafiki ndani na nje ya muziki. Maisha ni mafupi na siku Meek alipotoka jela alinipigia na tuliongea kwa muda wa lisaa,sio kuhusiana na beef bali ni kuanza mwanzo, mambo yajayo kitu gani kimetushika kwenye muziki wa Hip Hop. Sikuwahi kukutakia jela kamwe lakini ulipotoka nimepata furaha, niliongea hilo kwenye simu na naliongea tena, ‘karibu nyumbani’

Kwa upande wa Meek Mill alionyesha kuwa wapo sawa na The Game baada ya shabiki katika akaunti ya tweeter kuandika kwamba ‘kuna uwezekano kati yako na Game kufanya muziki?’ Meek akajibu kwa kuandika, “Ndiyo kwa nini isiwezekane

 

Bifu la Meek Mill na The Game lilianza mwaka 2016 baada ya The Game kuamini kwamba Meek ameiambia polisi kuwa alimwibia Sean Kingston vitu vyenye thamani ya Dola $300,000 (Sawa na Tsh. Million 690).

Comments are closed.