The House of Favourite Newspapers

INATISHA! KADA CHADEMA AUAWA NA MKEWE NA BINTIYE! – VIDEO

 

TUKIO ambalo ni gumzo katika Mji wa Morogoro maeneo ya Chamwino ni la mauaji ya kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ‘Chadema’ aliyefahamika kwa jina la Boniface Augustino ambaye anadaiwa kuuawa na mkewe aitwaye Neema Godfrey akishirikiana na bintiye na mtu mwingine ambaye jina lake halikufahamika, Ijumaa Wikienda lina ripoti ya kusikitisha kuhusu tukio hilo.

 

Mauaji hayo yaliyoacha simanzi na vilio yalitokea Mei 27, mwaka huu saa 7 mchana Mtaa wa Mwande ambapo inadaiwa kabla ya tukio hilo, marehemu alikuwa na mgogoro na mkewe, chanzo kikiwa hakifahamiki.

 

Kufuatia mauaji hayo, mwandishi wetu alifunga safari hadi eneo la tukio ili kujua undani wake ambapo alifanikiwa kukuta polisi wakiuchukua mwili wa marehemu pamoja na watuhumiwa kisha kuondoka eneo hilo huku wakiacha sintofahamu kwa wakazi wa eneo hilo.

MAJIRANI WAFUNGUKA

Wakizungunza na Ijumaa Wikienda kwa sharti la majina yao kutoandikwa gazetini, baadhi ya majirani walisema kuwa, walishangazwa na taarifa za mauaji hayo licha ya kwamba walikuwa wakijua kwamba marehemu na mkewe walikuwa hawako vizuri kimaelewano.

 

“Kwa kweli tukio hili limenisikitisha sana, huwezi kuhukumu moja kwa moja kwamba waliomuua Boni ni mkewe na mwanaye lakini kuna mazingira ambayo yanaashiria kuhusika kwao. “Niliwahi kusikia wako kwenye mgogoro hadi familia ikaingilia kati, sasa kuja kusikia haya mambo ya kifo, nilipigwa butwaa kwa kweli,” alisema jirani huyo.

 

MSIKIE SHUHUDA HUYU

Jirani mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Selemani Idd alisema kuwa, siku ya tukio alimsikia marehemu akilalama kuwa anauawa, asaidiwe huku purukushani zikitawala ndani ya nyumba, baadaye ukimya ukatawala.

“Marehemu alifanya hivyo kwa muda mchache baadaye tukaona kimya, tukasogelea eneo la tukio na kumuona mkewe na mwanaye pamoja na mpangaji wao aitwaye Juma wakiteta huku mtoto mkubwa wa Boni akiwa na wasiwasi, akawa anaingia ndani, anatoka.

“Tukatoa taarifa kwa mwenyekiti ambaye naye aliita sungusungu wa mtaa, walipoingia ndani walimkuta Boniface akiwa amefariki dunia akionekana amepigwa na kitu kizito kichwani, pembeni kulikuwa na mchi, ndipo polisi walipoitwa na kuuchukua mwili,” alisema Sele.

 

Mke adaiwa kujichanganya Sele alizidi kudai kuwa, mke wa marehemu baada ya kubanwa na Afisa Mtendaji wa Kata ya Chamwino, Bright Sospeter alidai eti mumewe wakati anapiga makele ya kuuawa alikuwa kachanganyikiwa na yeye hakuwepo.

 

“Baada ya mtendaji kumhoji mke alisema eti mume wake alirukwa na akili kipindi cha mchana na ndiyo maana alisikika akipiga kelele za kwamba anamuua, akasema eti kwa muda huo hakuwepo, tulishangazwa na maelezo hayo,” alizidi kufunguka jirani huyo.

 

MSIKIE DADA WA MAREHEMU

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, dada wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Esther Agostino Kibwanason alisema: “Boniface ni pacha wangu, mimi ni Kulwa, yeye Dotto, mimi naishi Dar na mume wangu naye alikuwa akiishi hapa na mke wake. Cha ajabu juzi nilipigiwa simu nikielezwa kwamba pacha wangu kauawa huku wauaji wakidaiwa kuwa ni mkewe, mwanaye na aliyekuwa mpangaji wao Juma.

“Kwa muda mrefu walikuwa kwenye mgogoro wa ndoa yao, mwezi uliopita wifi kanipigia simu akidai wako kwenye mgogoro huku chanzo kikiwa ni binti yao. Ni mauaji ambayo yameniumiza sana kwa kweli. Kwa kuwa hili suala liko polisi, acha tuache,” alisema Esther. Kamanda wa polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa wanaendelea na uchunguzi huku wakiwashikilia watu watatu kwa mahojiano zaidi.

TAZAMA VIDEO

Comments are closed.