The House of Favourite Newspapers

INAUMA SANA: Mtoto Asimulia Alivyotafunwa Mikono na Nguruwe – Video

Farida akiweka chai kwenye kikombe.

MTOTO Farida Silvanus (15), mkazi wa Perege Wiliya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani,amewashangaza watu kutokana na vitu anavyofanya huku akiwa ana mikono yote miwili.

 

Akizungumza na Global TV, Farida amesema kuwa alipata ulemavu huo wa kukatika mikono baada ya kung’atwa na Nguruwe akiwa na umri wa mwaka mmoja na nusu wakati mama yake alipokuwa ameenda kisimani kuchota maji.

 

Amesema, kuwa mama yake huyo alimuacha kitandani ndipo Nguruwe, aliposukuma mlango kwa kishindo kisha kumvuta kitandani na kumsokomeza uvunguni na kuanza kutafuna mikono yake yote miwili pamoja na kidevu.

 

Akisimulia zaidi mkasa huo, Farida amesema, baada ya mama yake kuona hivyo alipiga kelele na majirani walikuja na kuamua kunipelekea katika hospitali ya mkoa wa Iringa,ambapo alipatiwa matibabu hapo..

 

Japokuwa ana changamoto ya kukosa mikono yote mtoto Farida, anaweza kufanya kila kitu anachofanya mtu ambaye ana mikono yote miwili huku akitamani kupata mikono bandia.

INAUMA: Mtoto Asimulia Alivyotafunwa Mikono na Nguruwe

 

HADITHI: SIKU ZA MWISHO ZA UHAI WANGU – SEHEMU YA 1 (Audio)

Nakuletea dakika 15 za kwanza za simulizi hii tamu ya SIKU ZA MWISHO ZA UHAI WANGU. Ukitaka kuisikiliza simulizi hii Install #GlobalPublishersApp sasa. Utasoma na kusikiliza kitabu chote kuanzia sehemu ya kwanza hadi ya mwisho bureeeee!

Android: Bofya ==>http://bit.ly/2AAQe1d
iOS: Bofya ==>http://apple.co/2Assf4M

Comments are closed.