The House of Favourite Newspapers

Indonesia: Kaburi la urefu wa mita 100 kuzikwa watu 1,300

MAANDALIZI ya kuizika miili ya takribani watu 832 waliofariki baada ya nchi ya Indonesia kukumbwa na tetemeko la ardhi pamoja na Tsunami yameanza.

Hapo awali kikosi maalumu kilielekezwa kuandaa kaburi la miili 300 lakini maelekezo mapya yametaka kaburi hilo liwe kwa ajili ya watu 1,300

Aidha serikali imesema kuwa idadi ya waliofariki na kujeruhiwa huenda ikaongezeka kutokana na kutoonekana kwa watu wengi huku juhudi za kufukua vifusi zikiendelea.

Uduni wa vifaa vya uokoaji unaelezwa kuchangia kuchelewesha kutoa miili ya watu 60 iliyokwama kwenye vifusi vya jengo moja la hoteli iliyoanguka katika Jiji la Palu lenye watu wapatao 300,000 ambapo watu wengi zaidi wamepatikana wakiwa wamekufa.

A survivor picks through debris in badly-hit Palu
Moja ya sehemu zilizokumbwa na janga hilo.
A bridge has collapsed in Palu, where most of the dead have so far been found
Njia zinazotumiwa na waokoaji.

Rais wa Indonesia, Widodo, amekubali kupokea misaada kutoka nje baada ya kutembelea eneo hilo Jumapili ambapo ametaka zifanywe juhudi za usiku na mchana kukabili madhara ya tetemeko hilo lililokuwa na ukubwa wa ‘magnitude’ 7.5.

Comments are closed.