The House of Favourite Newspapers

MAJIZZO AMVALISHA LULU PETE YA UCHUMBA, NDOA IMEIVA!

MOJA ya stori zinazo-trendi kwenye social networks kwa sasa ni tukio la kihistoria la muigizaji wa filamu za Bongo Movie, Elizabeth Michael ‘Lulu’,  kuvishwa pete ya uchumba na mpenzi wake ambaye ni C.E.O wa EFM na ETV, Majizzo.

 

Tukio hilo la kuvalishwa pete limefanyika usiku wa jana Jumapili, Sepetemba 30, 2018 ambapo imesemekana kuwa lilikuwa ni surprise kwa mlimbwende huyo.

 

Imeelezwa kwamba, sherehe hiyo iliandaliwa na Majizzo maalum kwa ajili ya watoto wake, lakini mambo yalibadilika ghafla, ambapo wakati sherehe ikiendelea, watoto waliwaita mbele baba ambaye ni Majizzo na Aunt yao ambaye ni Lulu.  Shughuli ya kuvalishwa pete ikafanyika huku Lulu akiangua kilio kwa kutoamini surprise aliyofanyiwa na mpenzi wake huyo.

Lulu na Majizzo sasa wameamua kuweka mahusiano yao rasmi baada ya kuishi kwenye mahusiano hayo kwa siri na inaelezwa mipango ya ndoa inafanyika na huenda ikafungwa mwaka huu wakawa mke na mume.

Katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye anasemekana ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Harusi ya Majizzo na Lulu, alikuwepo kushuhudia tukio hilo.

Comments are closed.