The House of Favourite Newspapers

Instagram Yazindua Video ya Matangazo ya Moja kwa Moja (Live Streaming)

_92604952_live_instagram  

MTANDAO maarufu wa kijamii wa Instagram ndio mtandao wa huduma ya kijamii wa hivi karibuni kuzindua video za matangazo ya moja kwa moja (Live Streaming).

Mtandao huo umeamua kuboresha teknolojia yake kulinga na mahitaji ya sasa hasa matumizi ya video, ukifuata nyayo za mitandao wa facebook,unaomiliki Instagram,You Tube pamoja na programu ya moja kwa moja ya Twitter ya Periscope, Instagram imezindua programu mpya inayoruhusu wateja wake kuweka matangazo ya moja kwa moja wakati wowote.

_92607595_instagramlive2Mtu yeyote anayetazama anaweza kutoa maoni yake kwa kuweka emoji ambazo hujitokeza katika video hiyo ya moja kwa moja.

Inaonekana kuwa ya kawaida,lakini kuna tofauti kubwa.Mara tu unapomaliza kuweka matangazo yako hupotea kabisa.

_92604956_instagramvideoHiyo inamaanisha hutaweza tena kusambaza link ya video yako kwa wanaotazama na hawataweza kuiona tena baada ya matangazo hayo.

Katika taarifa ,msemaji wa Instagram alisema kuwa hiyo inalenga kuwafanya wateja kuhisi faraja na kuweza kusambaza chochote wanachotaka kusambaza.

Programu hiyo itasambazwa kwa kundi la wateja wa mtandao huo kabla ya kutumika na kila mtu katika kipindi cha wiki chache zijazo.

Comments are closed.