The House of Favourite Newspapers

TMA: Mvua za Uwepo wa LANINA Kunyesha Hadi Desemba

tma

DAR ES SALAAM: Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema mvua za vuli zinazoendelea kunyesha nchini ni mvua ambazo kama wananchi hawatachukua tahadhari za haraka zinaweza kuleta madhara makubwa.

Hayo yamesemwa na Meneja Kitengo Kikuu cha Utabiri cha Mamlaka hiyo, Bw. Samwel Mbuya wakati akitoa ufafanuzi wa mvua zinazoendelea kunyesha nchini na kusababisha madhara kwa baadhi ya mikoa.

Amesema mabadiliko ya hali ya hewa kwa sasa yanatokana na kuwepo kwa msimu unaotawaliwa na uwepo wa LANINA ambayo ni ongezeko la hali ya baridi katika eneo la Ikweta ya Bahari ya Pacifiki.

Amesema bado matarajio ya vipindi vifupi vya mvua kubwa na upepo vitaendelea kuwepo katika msimu huu mpaka mwezi Desemba na mabadiliko kidogo yatajitokeza kwa baadhi ya mikoa ambapo mvua zitanyesha kwa wastani.

Akizungumzia hali ya joto amesema itaongezeka kwa baadhi ya mikoa hasa ya Dar es Salaam itaendelea kuwepo kwa kipindi kirefu.

Kuhusu watumiaji wa vyombo vya bahari amewatahadharisha kuzingatia taarifa za hali ya hewa ili kuepusha madhara ambayo yanaweza kutokea kama taadhari hizo hazitazingatiwa.

halotel-strip-1

Comments are closed.