The House of Favourite Newspapers

ISAAC GAMBA ALIVYOAGWA LEO DAR

 Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo (kulia) na waombolezaji wengine wakilipeleka jeneza lenye mwili wa Isaac Gamba sehemu ya kuagiwa.

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda,  leo amewaongoza waombolezaji waliojitokeza katika hospitali ya jeshi la Lugalo jijini Dar es Salaam kuuaga mwili wa aliyekuwa mtangazaji wa idhaa ya kiswahili ya Ujerumani DW, Isaac Gamba. Mwili huo baada ya ya kuagwa ulipelekwa Uwanja wa ndege wa Julius Nyerere kwa ajili ya kusafirishwa mpaka Mwanza na kisha kupelekwa Bunda, Serengeti, mkoani Mara kwa ajili ya mazishi.

Mhariri Mtendaji wa Global Publishers Ltd, Saleh Ally (mwenye miwani) akiwaongoza waombolezaji waliobeba jeneza lenye mwili wa  Gamba.

Ofisa wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) akimsalimia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Mkuu wa Ulinzi na Usalama wa mkoa huo, Paul Makonda.  Kulia ni mtangazaji maarufu nchini na nchi za nje, Charles Hillary aliyewahi kufanya kazi na marehemu Gamba.

Bosi wa zamani wa marehemu Gamba alipokuwa Radio One, Joyce Mhavile (kulia) akisalimiana na aliyekuwa bosi wa Gamba katika kituo cha redio cha DW  cha Ujerumani mpaka alipopatwa na umauti.    Makonda akitoa heshima za mwisho kwa marehemu.

 Mkuu wa Kitengo cha Global TV Online, James Range (mwenye miwani) akitoa heshima za mwisho.

Msemaji wa Klabu ya Simba ya Dar es Salaam, Haji Manara (kushoto) akitoa heshima za mwisho.

Mmoja wa waombolezaji akilia kwa uchungu wakati wa kutoa heshima za mwisho.

Waombolezaji wakiwa kwenye msululu wa kwenda kuaga.

Rafiki wa marehemu na aliyekuwa mfanyakazi mwenzake DW, Sudi Mnette,  akiwaeleza wanahabari jinsi alivyoishi na Gamba nchini Ujerumani mpaka alipofariki dunia.

 

PICHA: RICHARD BUKOS / GPL

 

Comments are closed.