The House of Favourite Newspapers

Isha Mashauzi: Jimbo Lipo Wazi, Natafuta Mchumba – Video

Isha Mashauzi akiwa ndani ya studio za +255 Global Radio akifanya mahojiano na kipindi cha Jahazi la Pwani.

MWIMBAJI wa muziki wa taarabu Bongo, Isha Mashauzi, amesema anatafuta mume wa kumuoa baada ya kuachika katika ndoa yake ya pili.

 

Mwimbaji huyo alisema hayo wakati alipokuwa akifanya mahojiano na kipindi cha Jahazi la Pwani kinachorushwa na 255 Global Radio.

“Jimbo liko wazi, nimewahi kuolewa mara mbili mume wangu wa kwanza nimezaa naye mtoto mmoja, na mume wangu wa pili hatukubahatika kupata naye mtoto, waume zangu wote tulihitilafiana kila mmoja akaenda kutengeneza maisha yake.

“Sasa hivi niko mwenyewe natafuta mtu,” alijibu Aisha baada ya kuulizwa swali kuwa kumekuwa na tetesi za yeye kuolewa na waume wa watu.

MWIMBAJI wa muziki wa taarabu nchini, Isha Mashauzi, akiwa katika picha ya pamoja na mtangazaji wa kipindi cha Jahazi la Pwani, Odo Aisha.

Aidha, aliendelea kwa kusema,“Wanitafute, nahitaji nipate mtu atakayenienzi, atakayenipenda, sijali kuhusu muonekano wake, lakini tu awe na kipato cha kuweza kunisaidia na familia yangu. Nataka kweli sio kwamba natania, mimi ni mzuri wa kila kitu, wanitafute,” alisisitza Isha.

Comments are closed.