The House of Favourite Newspapers

Ishu Ya Rosa Ree Kusainiwa Kwenye Lebo ya Rapa Rick Ross Iko Hivi…Ukweli Upo Hapa

0
Rapa mkali wa kike Bongo, Rosa Ree.

 

ROSA REE; ni rapa mkali wa kike Bongo ambaye amefunguka kuhusu ishu ya kusainiwa kwenye lebo ya rapa mkubwa wa Marekani, Rick Ross iitwayo Maybach Music Group.

 

Rosa Ree anasema anafurahia kuona Rick Ross amekubali muziki wake na mambo yatakapokuwa tayari mashabiki wake watafahamu.

 

“Kiukweli nashukuru kuona Rick Ross mtu ambaye nimekuwa nikimsikiliza tangu nipo shule anakuwa anakubali kitu ambacho nakifanya, hata nilipotoa wimbo wangu wa mwisho, Blue Print alitoa maoni kwamba ni kitu kizuri.

 

“Mambo ni mazuri kwa sababu tunawasiliana, tunaongea na huwezi kujua yajayo yanaweza kuwa ni makubwa sana, sitaki kufichua chochote napenda mfahamu ni kitu gani kitakuwepo huko mbele pindi tutakapokuwa tayari,” anasema Rosa Ree.

 

Hivi karibuni, Rick Ross au Madevu, akiwa kwenye ziara ya kimuziki barani Afrika aliweka wazi kuvutiwa na wasanii watatu barani humo na mmojawao akiwa ni Rosa Ree.

STORI NA SIFAEL PAUL | IJUMAA WIKIENDA @sifaelpau

MO AMWAGA MAMILIONI SIMBA, VYUMA VYAANZA KUSHUSHWA, HERSI AFICHUA USAJILI YANGA | KROSI …

Leave A Reply