The House of Favourite Newspapers

ISHU YA YOUNG D, AMBER LULU YAFIKA PABAYA

David Genzi ‘Young Dee’

MSANII wa Muziki wa Bongo Fleva, Lulu Eugen ‘Amber Lulu’ amejikuta akiingia katika bifu zito na msanii mwenzake, David Genzi ‘Young Dee’ baada ya kumtolea maneno ya shombo katika ukurasa wake wa Instagram kwa kusema kwamba rapa huyo hawezi kuoa kwa sababu hicho si kitendo rahisi na ukiangalia yeye mwenyewe sasa hivi anatamani

kuolewa, hivyo kumtaka afanye muziki bila kutengeneza kiki kama anaweza. Maneno hayo ya Amber Lulu yalitokana na picha ya harusi iliyokuwa ikisambaa mitandaoni, huku watu na mastaa mbalimbali wakidai kuwa rapa huyo ameamua kuoa kimyakimya bila kumualika mtu yoyote

Akizungumza na Vijistori Mitandaoni, meneja wa Young Dee alisema kuwa; “Young Dee hawezi akabishana na mtoto wa kike halafu hata hivyo huyo Amber Lulu hawezi akafanya muziki mzuri bila kufanya kiki na tena ukiangalia kiki zake nyingi ni lazima amtaje Young Dee, kwa sababu anajua kuwa brand kubwa hivyo anaona akimtumia lazima atoboe,” alisema meneja huyo.

Amber Lulu naye huyu apa; “Niliongea vile kwa sababu najua Young Dee hawezi akatoa wimbo bila kufanya kiki, anadanganya watu kuoa wakati yeye mwenyewe anahitaji mtu wa kumuoa, halafu ukiangalia kiki ni kubwa kuliko wimbo anaotaka kuutoa yani kiufupi siku hizi muziki wake ushakufa labda ajipange upya,” alisema Amber Lulu.

Na Memorise Richard

Comments are closed.