The House of Favourite Newspapers

Israel na Palestina Zakubaliana Kusitisha Mapigano katika Ukanda wa Gaza

0
Mlipuko ukanda wa Gaza

ISRAEL na Palestina zimefikia makubaliano ya kusitisha mapigano katika ukanda wa Gaza kufuatia mashambulizi yaliyotekelezwa na majeshi ya Israel kuelekezwa kwa wanamgambo wa dola ya kiislam yaliyosababisha kuuawa kwa raia 44 wa Kipalestina.

 

Imeripotiwa kuwa zaidi ya watoto 15 kati ya raia 44 wameuawa katika shambulio hilo ambalo kwa mujibu wa Serikali ya Israel ilisema kuwa shambulio hilo liliwalenga wanamgambo wa dola ya kiislamu akiwemo Kamanda wao Mkuu, huku Palestina wao wakikanusha madai hayo na kusema kuwa mashambulizi ya Israel yamelenga kambi za wakimbizi.

Waokoaji nchini Palestina wakiendelea na shughuli za uokoaji

Aidha licha ya Mataifa yote kukubaliana katika dhana ya kusitisha mapigano, kila mtu amemuonya mwenzie kuwa ataweza kufanya mashambulizi ya haraka endapo tu machafuko yatatokea.

Waandamanaji nchini Palestina

“Serikali imetangaza kufunguliwa kwa Ofisi mbalimbali lakini pia Vyuo Vikuu navyo vimetangaza kufunguliwa kwa ajili ya wanafunzi. Manispaa ya Gaza pamoja na Manispaa nyingine nazo zimetangaza kupeleka vifaa ili kuondoa vifusi vilivyosababishwa na mashambulio ya siku tatu.” Amekunukuliwa akisema mwandishi wa habari wa Aljazeera Safwat al-Kahlout.

 

 

Leave A Reply