Itel Yawatoa Out ‘Valentine Dinner’ Wataje Wake

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Itel Tanzania imefanya droo yake ya kwanza hivi karibuni  katika promosheni inayoendelea kwa jina la “Nogesha Valentine na itel”

Akiwatangaza washindi jijini  Dar es Salaam meneja mauzo kanda ya Dar es Salaam Bwana Cleophas Mapunda alisema wanatimiza ahadi ya kile walichoahidi tangu kuzinduliwa kwa promosheni hiyo mwanzoni mwa mwezi huu wa Februari.

“Mshindi wa kwanza ni Nashon mwenye vocha namba 00827 na namba yake ya simu ni……… huuyu amejishindiia kwenda Valentin dinner na ampendaye katika hotel nzuri, washindi wengine wawili ni Happy vocha namba yake ya bahati nasibu ni 00710 na namba yake ya simuu ni 07547507.. na Zawadi ambaye vocha namba yake ni 00399 na namba yake ya simu ni 07733128…hawa wamejishindia rice cooker kila mmoja pamoja na vitu vingine vya matumizi ya nyumbani” alisema Mapunda.

Meneja mauzo wa itel kanda ya Dar es Salaam Bw. Cleophas Mapunda akimkabidhi zawadi ya ricecooker mshindi Happy katika droo ya kwanza

Mapunda aliongeza kuwa promosheni hiyo inaendelea katika mwezi mzima wa wapendanao yaani Februari huku akisisitiza kuwa wateja wanaonunua itel A56, S16, na A35 wataingia moja kwa moja katika droo ya kushinda zawadi nyingine kubwa katika awamu mbili  zilizobaki za kuchezeaha droo.

 

“Droo yetu nyingine tunatarajia kuchezesha Februari 23 na Februari 27 ambapo tarehe 23 mshindi atapata TV ya ite yenye inchi 32 na mshindi wa tarehe 27 atapata TV ya itel yenye inchi 43, kwahiyo tunawahimiza Watanzania kununua simu zetu ili kupata kitu kingine zaidi ya simu katika msimu huu wa wapendanao”

Msimamizi wa duka la itel Kariakoo Jijini DSM Bi. Dotto akimkabidhi zawadi ya ricecooker mshindi wa Droo ya kwanza Bw. Zawadi.

Msimamizi wa duka la itel Kariakoo Jijini DSM Bi. Dotto akimkabidhi zawadi ya ricecooker mshindi wa Droo ya kwanza Bw. Zawadi.

Promosheni hiyo ya itel inayokwenda kwa jina la “Nogesha Valentine na itel” ilizinduliwa rasmi mwanzoni mwa mwezi huu wa Februari na meneja mahusiano wa itel Tanzania Bwana Fernando Wolle na itahitimishwa Februari 28.

Taarifa zaidi tembelea kurasa za itel, Facebook itel TZ na instagram   https://www.instagram.com/

Toa comment