The House of Favourite Newspapers

Jahazi Kuja kwa Kishindo Mkesha wa Krismasi

Stori: RISASI BMM

KUNDI bora la Muziki wa Taarab, Jahazi Modern Taarab linatarajiwa kuja kwa kishindo mkesha wa Sikukuu ya Krismasi (Desemba 24, mwaka huu) ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.

Akizungumza na Risasi BMM, Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo alisema kuwa, usiku huo utakuwa wa kihistoria kwa maana kutakuwa na sapraiz ambayo haijawahi kutokea tangu kundi hilo lianzishwe.

“Wakali kibao watakuwepo wakiongozwa na Malkia Leyla Rashid na Amigo. Utakuwa usiku wa weka kitu toa kitu,” alisema Mbizo.

Comments are closed.